LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 24, 2019

WATU 2000 WAFARIKI DUNIA KUTOKANA NA EBOLA NCHINI DRC

Mike Ryan, mkuu wa masuala ya dharura katika WHO, ameeleza wasiwasi wake kuhusu kuenea kwa ugonjwa wa Ebola nchini DRC. Aidha amesema katika kukabiliana na Ebola nchini DRC, WHO inahitaji msaada wa dola milioni 278.
Mwezi Julai mwaka huu Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitangaza ugonjwa wa Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuwa ni ''dharura ya kiafya inayohitaji kutazamwa na kupewa mazingatio na jumuia ya kimataifa''.
Hatua hiyo inaweza kuzifanya nchi tajiri zinazotoa msaada kutoa fedha zaidi kukabiliana na ugonjwa huo. Lakini shirika hilo limesema hatari ya ugonjwa huo kusambaa nje ya Congo si kubwa.
Uamuzi wa kutangaza ugonjwa wa Ebola kuwa dharura ya kiafya duniani ulichukuliwa na jopo la wataalamu wa Shirika la Afya Duniani katika hali ambayo wasiwasi wa kusambaa ugonjwa huo umeongeza zaidi katika siku za hivi karibuni.
Mapema mwezi Agosti kuligunduliwa kesi zaidi za maambukizi ya Ebola katika mji wa Goma  na hivyo kuzidisha wasiwasi wa kuenea zaidi ugonjwa huo kwenye eneo hilo lenye idadi kubwa ya watu ambalo liko umbali wa kilomita zaidi ya 350 kutoka mahala ugonjwa huo ulipogundulika kwa mara ya kwanza Agosti mwaka jana katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Eneo la kuwatibu watu wanaougua ugonjwa wa Ebola
Kwingineko,  hivi karibuni taarifa ya WHO ilieleza kuwa zoezi la utoaji chanjo linaloendelea sasa limefikia kiwango cha asilimia 98. 
Mbali na DRC zoezi hilo la kutoa chanjo ya Ebola pia linafanyika katika nchi jirani za Burundi na Uganda.
Ikumbukwe kuwa, mfumuko mkubwa zaidi wa ugonjwa wa Ebola ulitokea baina ya Disemba 2013 na Aprili 2016 na kuua zaidi ya watu 11,000 katika nchi za Guinea, Liberia na Sierra Leone huko magharibi mwa bara la Afrika.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages