Kundi linalojiita jeshi la kitaifa la Libya linaloongozwa na Kamanda Khalifa Haftari jana Jumamosi liliushambulia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mitiga mashariki mwa Tripoli mji mkuu wa nchi hiyo.
Mashambulizi hayo yamesababisha kusitishwa safari za ndege katika uwanja huo. Mapigano yameshuhudiwa kupambana moto hivi karibuni kati ya wanamgambo hao wanaoongozwa na Jenerali Khalifa Haftar na vikosi vya serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Libya kusini na mashariki mwa mji mkuu, Tripoli. Kundi hilo linalojiita jeshi la kitaifa la Libya ambalo kwa miaka kadhaa sasa linaungwa mkono na Saudi Arabia, Misri, Imarati na baadhi ya nchi magharibi na ambalo lilikuwa likiyadhibiti maeneo ya mashariki mwa Libya miezi kadhaa ya karibuni limesonga mbele kuelekea upande wa kaskazini mwa nchi. Aidha tarehe nne Aprili mwaka huu Khalifa Haftar aliwaamuru wapiganaji wake kuushambulia mji mkuu wa Libya, Tripoli; hatua iliyolaaniwa na jamii ya kimataifa.
Watu zaidi ya 1000 wameuawa katika mji wa Tripoli na wengine wasiopungua 5,500 wamejeruhiwa tangu kuanza mapigano kati ya pande mbili hizo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇