LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 11, 2019

WANAJESHI KIGOMA WATAKIWA KUKAAGUA USALAMA MPAKANI MAGHARIBI


Na Rhoda Ezekiel Kigoma,

MKUU wa Brigedi ya magharibi 202 KV, Brigedia jenerali Jackobo  Mkunda amewataka Wanajeshi wa Kikosi cha 24 Kj, kuhakikisha Wanaendelea kukaa na kukagua ulinzi na usalama katika Ofisi zao ambazo ni Mapori ya Mkoa wa Kigoma ilikuhakikisha mpaka wa magharibi unakuwa salama na hauvamiwi na watu waovu.


Wito huo aliutoa jana wakati wa kihairisha Mafunzo ya siku 13 yaliyofahamika kama Zoezi Kikaka, yaliyo husisha kombania kjjifunza namna ya kukabiliana na maadui, kuainisha matumizi ya silaha  za kivita ,kutathimini utendaji kazi wa silaha za kikosi,kuimalisha utendaji kazi wa kikosi kuwezesha  maafisi   kujua  matumizi ya silaha  za kivita katika nyakati zote na kuwajengea uwezo maafisa wa kutoa amri na matumizi ya redio nyakati za vita.


Alisema Zoezi hilo litakuwa endelevu na hawatakubali kuona misitu na mapori yanavamiwa na Raia kutoka Nje ya Nchi, wanaotumia mapori hayo kufanya uharifu na kuwatishia usalama Wananchi wa Mkoa wa kigoma, jeshi litahakikisha linalinda amani na usalama wa maeneo hayo kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama.

Brigedia Mkunda alisema ilikuhakikisha Wanamuunga mkono Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, katika adhima yake ya Uchumi wa Viwanda ni lazima wahakikishe Nchi iko salama na wananchi wanafanya Shughuli zao bila kuwa na bugha yoyote na kuhakikisha amani inaendelea kuwepo.


"Kazi ya kuhakikisha ofisi zao ziko salama ni haki yao askari wa Jeshi la Wananchi hivyo  kuzijua ofisi zao na wanapaswa kuzilinda na kuhakikisha muda wote ziko salama , kwa kipindi chote cha mafunzo wameweza kujiimarisha vizuri zaidi na zoezi hilo ni endelevu nipende kuwahakikishi Wananchi kuwa eneo hilo ni salama na wafanye kazi kwa uhuru', alisema brigedia Mkunda.

Alisema suala la ulinzi na usalama sio la Jeshi pekee kila taasisi pamoja na Wananchi wanatakiwa kuwafichua Watu wote wanaoingia  Nchini bila vibali na kufanya uharifu pamoja na raia wanaoshirikiana nao katika vitendo hivyo.

Nae Mkuu wa mafunzo  na utendaji  kivita kikosi 202KV  Kanali Wilson Ibuge alieleza kuwa mapori yanapoonekana hayana watu yana mwenyewe na mwenyewe ndio Jeshi la Wananchi na zoezi ndio kwanza limeanza,  kazi ya jeshi ni vita hawapendi vita na iliwaweze kutekeleza vita lazima wajiandae na sehemu pekee ni mafunzo ya kivita na mazoezi.

Alisema Matarajio ya brigedi sio tu eneo la miliki ya kikosi cha 24 kj zoezi hilo ni endelevu na linapeleka salamu kwa wavamizi wa maeneo hayo na wakitaka salama ni kuacha kujihusisha na mambo ya kijangili na uharifu  na pamoja na Wananchi wa Tanzania wanaoshirikiana na Watundi kufanya uharifu wote  watashughulikiwa ipasavyo.

 Aidha kamanda wa kikosi cha 24 KJ Meja Jonson Luhovyq alisema.kuwa ndani ya siku kumi na tatu za mafunzo hayo Askati wameweza kufanya zoezi hilo katika maeneo ya Malagarasi, Mvugwe, Kagerankanda, Busunzu,Nyarugusu na Kisogo pamoja na maeneo yanayo karibia kambi ya Kanembwa.

Alisema katika zoezi hilo waliweza kubaini baadhi ya raia kutoka Nchi jirani ya  Burundi, kuwepo katika eneo la mapori hayo wanaojihusisha na Uvunaji wa mihogo baada ya hapo wanajihusisha na mambo mengine ya kiharifu .

Alisema watahakikisha Wanalinda maeneo hayo pamoja na askari kufanya mafunzo hayo wataweza kushirikiana na Jeshi la polisi kulinda amani ha maeneo ya mpakani, na katika zoezi hilo matokeo makubwa yamepatikana na litakuwa endelevu.


Hata hivyo alisema Changamoto waliyonayo ni ukosefu wa mafuta, endapo wakipata lita 300 kila mwezi, wataweza kuendelea na mazoezi hayo katika mapori ilikuhakikisha maeneo hayo yanakuwa salama na hakuna uharifu.


Aidha mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma  ambae pia ni Mkuu wa Eilaya ya Kasulu Kanali  simon Hanange aliwapongeza askari kwa kazi kubwa walioifanya, na kuswma kwamba poti hilo lazima lilindwe kwa kuwa eneo kubwa la pori hilo ni chanzo cha  mto Maragalasi linalomwaga maji katika Ziwa Tanganyika endapo litahaeibiwa litasababisha kuongezeka kwa joto ziwani na kusababisha  madhara pamoja na samaki kukimbia.


Alisema serikali inampanho wa kuboresha bandari ya Mkia wa kigoma ni lazima zipwa liendelee kulindwa na kuwa la kisasa kwa kuwa  bandari inategemea ziwa kazima msitu huo ulindwe, serikali itaendelea kushirikiaka na jeshi jkuhakikisha katika mapori hayo  hakuna kilimo kinachofanyika wala  kuwepo na vitendo vya uharifu.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages