Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt. Respicious Boniface akizungumza jambo wakati wa hafla ya kupokea chumba maalum cha upasuaji kwa watoto wenye vichwa vikubwa na Mgongo wazi MOI
Dkt. Wonanji Vivian (kushoto) akikata utepe kuashiria kupokea chumba maalum cha upasuaji cha watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi katika Taasisi ya MOI iliyofanyika leo Agosti 26, 2019
Wajumbe wa kamati ya uendeshaji ya MOI (Management comitee) ya MOI pamoja na wadau wengine wakifuatilia hotuba katika hafla ya kupokea chumba maalum cha upasuaji cha watoto wenye vichwa vikubwa na Mgongo wazi MOI leo.
Dkt. Wonanji Vivian akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi mtendaji wa MOI Dkt. Respicious Boniface wakiwa pamoja na wajumbe wa kamati ya uendeshaji ya MOI pamoja na Wadau mbalimbali wa MOI.
Dkt. Wonanji Vivian (wanne kushoto) katika picha ya pamoja na viongozi mblimbli wkiwemo na wadau.
Dar es Salaam, 26/08/2019. Mkurugenzi Msaidizi wa huduma za Umma na binafsi wa Wizara ya Afya maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Wonanji Vivian leo amepokea chumba maalum cha upasuaji wa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi ambacho kimekarabatiwa na MOI pamoja na wadau kwa zaidi ya Tshs Milioni 500.
Dkt. Wonanji amewashukuru wadau, wafadhili pamoja na washirika wa MOI ambao wameshiriki katika ukarabati na uanzishaji wa chumba hicho maalum.
“Leo tumekusanyika hapa kwa lengo moja kuu la kupokea rasmi chumba cha upasuaji kwaajili ya Watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi, hii ni hatua kubwa hapa nchini, nafahamu chumba hicho kilishaanza kutumika lakini leo kinakabidhiwa rasmi hongereni na ahsanteni wote mlioshiriki katika hili.” Alisema Dkt Wonanji.
Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt. Respicious Boniface amesema chumba hicho kimejengwa kwa ushirikiano na wadau mbalimbali ambao ni chama cha Wazazi wenye watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi Tanzania ASBATH, Ndugu AKheri Kakoo kutoka Shia khoja athna asheri Muslim community, Cure International na Ubalozi wa Kuwait hapa nchini.
“Chumba hiki kilianza kutumika mwezi Aprili na tayari watoto zaidi ya 352 wamefanyiwa upasuaji, ni matumaini yetu kwamba tutawahudumia watoto wengi zaidi ,awali tuliwafanyia upasuaji watoto 45-50 kwa mwezi sasa hivi tunawafanyia upsauji watoto 85-100 kwa mwezi hii imeondoa changamoto ya kusubiri upasuaji kwa muda mrefu.” Alisema Dkt. Boniface.
Mwenyekiti wa Chama cha Wazazi wenye vichwa vikubwa na Mgongo wazi Tanzania. Abdulhakim Bayakub amesema Takwimu zilizopo zinaonyesha kwamba zaidi ya watoto 4800 wanazaliwa na tatizo la kichwa kikubwa na mgongo wazi kila mwaka hapa nchini, ambapo idadi ya watoto wanakwenda hospitali kupata huduma imeongezeka maradufu kutokana na uelewa kuongezeka. Imetolewa.
Kitengo cha Uhusiano MOI
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇