LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 8, 2019

PENTAGON YAKABIDHISHA MADAI YA TRUMP

Rais Donald Trump wa Marekani tarehe 19 Disemba 2018 alitangaza kuwa, askari wa Marekani wataondoka nchini Syria. Trump alidai kuwa, sababu ya uamuzi huo ni kushindwa kundi la kigaidi la Daesh nchini Syria.
Katika hatua ya baadaye ikulu ya Rais wa Marekani, White House, tarehe 22 Machi mwaka huu wa 2019 ilitoa taarifa ikitangaza kuwa kambi ya mwisho kabisa ya kundi la Daesh nchini Syria imetekwa na kukamatwa. 
Hata hivyo Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon) Alfajiri ya Jumatano tarehe 7 Agosti imetangaza kuwa kundi la kigaidi la Daesh lingali linafanya harakati katika nchi za Iraq na Syria na linaendeza operesheni zake katika nchi mbalimbali. Mtandao rasmi wa Wizara ya Ulinzi ya Marekanii umenukuu ripoti ya mkaguzi wa "Operation Inherent Resolve" (OIR) akisema: Daesh inawahamisha wapiganaji wake huko Syria na kujiimarisha zaidi nchini Iraq. Operesheni hiyo ya OIR ambayo Marekani ilidai ni kwa ajili ya kulisambaratisha kundi la kigaidi la Daesh, ilianza Agosti mwaka 2016 na ingali inaendelea. Tathmini ya timu ya Operation Inherent Resolve ya jeshi la Marekani, inasema kwa sasa kuna wapiganaji karibu elfu 14 hadi 18 wa Daesh katika nchi za Iraq na Syria na zaidi ya elfu tatu miongoni mwao ni raia wa kigeni waliojiunga na kundi hilo.
Wapiganaji wa kundi la kigaidi la Daesh
Ripoti hiyo ya Pentagon inakadhibisha madai ya Donald Trump kuhusu kushindwa na kusambaratika kundi la Daesh. Trump amekuwa akidai kuwa, Marekani italiangamiza kundi hilo na inawahakikishia wananchi kwamba itawalinda mbele ya mashambulizi ya kigaidi. Hata hivyo madai hayo ni kinyume na uhakika wa mambo. Wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka 2016, Trump alisema kuwa, serikalii ya Barack Obama ndiyo iliyoanzisha kundi la kigaidi la Daesh. Kauli hii ina maana kwamba, serikali ya Marekani ndiye mwasisi na mfadhili mkuu wa kundi hilo la kigaidi. 
Baada ya kuanza mgogoro wa Syria mwaka 2011, Marekani ikiongoza muungano wa nchi za Kimagharibi na Kiarabu, ilitumia kundi la Daesh na makundi mengine ya kigaidi kwa ajili ya kutimiza malengo yake nchini humo badala ya kukabiliana na ugaidi na makundi hayo yenye misimamo ya kufurutu ada. Ivan Ipolitov ambaye ni mtaalamu wa masuala ya siasa anasema: "Katika miaka ya hivi karibuni Marekani imekuwa ikiyatumia makundi ya kigaidi na yenye misimamo mikali kwa ajili ya kutimiza malengo na siasa zake za nje, na matokeo ya hatua hiyo ni kudhoofishwa nchi za Mashariki ya Kati na kutayarisha mazingira ya kustawi zaidi ugaidi na makundi yenye misimamo ya kufurutu mipaka."
Wapiganaji wa Daesh wakiua watu kwa umati, Iraq
Utendaji wa Marekani nchini Syria unaonesha kuwa, tangu mwaka 2011 hadi 2014 wakati Daesh ilipovamia baadhi ya maeneo ya Syria na kutwaa baadhi ya miji ya Iraq, Wamarekani wamekuwa wakiwafadhili magaidi hao kwa silaha na fedha. Kuanzia mwezi Juni mwaka 2014 wakati ulipoundwa eti muungano wa kimataifa wa kupambana na Daesh, Marekani ilijikita zaidi katika kulilinda kundi hiilo katika eneo maalumu linalodhibitiwa na Wamarekani ili iweze kuwatumia wapiganaji wake dhidi ya serikali ya Syria na waitifaki wake. Suala hili lilizusha alama nyingi za kuuliza kuhusu madai ya Marekani na washirika wake ya eti kupambana na ugaidi hususan kundi la Daesh. Hasa ikitiliwa maanani kwamba, kabla ya hapo Donald Trump alikuwa amesema waziwazi kwamba, mapambano ya Marekani dhidi ya kundi la Daesh nchini Syria yatazinufaisha nchi za Russia na Iran na akahoji ni kwa nini basi Washington igharamie mapambano kama hayo yanayowanufaisha maadui zake? 
Ukweli ni kwamba, katika kipindi chote cha miaka 8 iliyopita, Marekani imekuwa mfadhili na muungaji mkono mkubwa wa makundi ya kigaidi yanayoipinga serikali halali ya Syria kwa shabaha ya kuiondoa madarakani lakini haijafanikiwa kufikia malengo yake. Washington inayatumia makundi ya kigaidi kama wenzo na fimbo ya kukabiliana na wapinzani wa siasa na sera zake na kwa msingi huo inafanya kila liwezekanalo kulinda mabaki ya kundi la Daesh kwa ajili ya kuyatumia katika malengo yake kwenye nchi kama Syria na Iraq.  

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages