LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 31, 2019

PAKISTAN WAANDAMANA NCHI NZIMA KULAANI UKATILI WA INDIA DHIDI YA WAISLAMU WA KASHMIR

Wananchi wa Pakistan wamefanya maandamano ya nchi nzima kulaani ukatili unaofanywa na serikali ya India dhidi ya Waislamu wa Jamu na Kashmir linalodhibitiwa na India.
Shirika la habari la IRNA limeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, wananchi wa Pakistan wamefanya maandamano hayo katika miji mbalimbali ukiwemo mji mkuu Islamabad wakiitaka serikali ya India iondoe hali ya hatari huko Jamu na Kashmir na iache kufanya ukatili dhidi ya wananchi wa eneo hilo.
Rais Arif Alvi wa Pakistan pamoja na Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Imran Khan wamehutubia maandamano hayo mjini Islamabad na sambamba na kuunga mkono haki za wananchi wa Kashmir wamesisitiza kuwa, Pakistan itaendelea kuunga mkono kisiasa na kidiplomasia mapambano ya wananchi wa Jamu na Kashmir hadi watakapojikomboa na kujiainishia wenyewe mustakbali wao.
Maandamano ya wananchi wa Kashmir kulaani ukatili wanaofanyiwa wananchi wa eneo la Kashmir lililoko chini ya udhibiti wa India

Waziri Mkuu wa Pakistan ameulaumu Umoja wa Mataifa na taasisi za kimataifa kwa kushindwa kuwasaidia wananchi wa eneo la Kashmir linalodhibitiwa na India na kutahadharisha kwamba hakuna fursa yoyote ya kufanyika mazungumzo baina ya Pakistan na India bali uwezekano wa kutokea mapigano baina ya nchi hizo mbili ndio mkubwa.
Kwa upande wake Rais Arif Alvi wa Pakistan ametangaza uungaji mkono wake kwa wananchi wa eneo la Kashmir linalodhibitiwa na India na kusema kuwa, Kashmir na Pakistan ni nchi moja isiyoweza kutenganishwa na dola lolote lile ulimwenguni.
Hivi karibuni serikali ya India ilivunja utawala wa ndani wa eneo la Kashmir lililoko chini ya udhibiti wake kama njama za kulidhibiti kikamilifu eneo hilo la Waislamu.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages