LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 12, 2019

NAIBU GAVANA BOT AZITAKA TAASISI ZA KIFEDHA KUZINGATIA UADILIFU

Na  Ferdinand Shayo,Arusha.


Naibu Gavana wa benki kuu Tanzania (BOT) Dr.Bernard Kibesse  amezitaka taasisi za kifedha kuzingatia uadilifu katika utoaji wa huduma za kifedha hasa katika zama hizi za kidigitali ili kuwahahikishia wateja wao usalama wa fedha zao.

Akizungumza katika  kongamano LA
 Taasisi za kifedha za Afrika Mashariki linaloendelea jijini Arusha ,Naibu Gavana amesema kuwa licha ya changamoto za wizi kwa njia za mitandao bado taasisi hizo zina jukumu la kufanya kazi kwa uaminifu na uadilifu Mkubwa kwani ndio nguzo kuu ya huduma hizo.

Aidha amesema kuwa serikali haitasita kuwachukulia hatua taasisi za kifedha zinazokiuka sheria ,maadali na tararibu za utoaji wa huduma ikiwemo kuzinyang'anya leseni .

Patrick mwisusa ni  mkurugenzi mtendaji wa  Tanzania institute of bankers amesema kuwa kongamano hilo linalenga kuangalia masuala ya nafasi ya maadili katika utoaji wa huduma za kifedha na kuhimiza suala la uadilifu katika kulinda tasnia ya fedha Katika nchi za Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla.

Mshiriki wa kongamano  ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Tasisi za Kifedha nchini Kenya  Kenya,  Gilbert Allela amesema kuwa taasisi za fedha zina nafasi Mkubwa ya kulinda na kutunza uaminifu wa wateja wao kwa kujifunza mbinu za kisasa za kukabiliana na wizi wa kimtandao.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages