Na John Walter Babati, Manyara
Mshindi wa kwanza kwenye mashindano ya kusaka vipaji vya kuimba mkoani Manyara,Prisca Gretu amerudisha Shukrani kwa Mkuu wa wilaya ya Babati Elizabeth Kitundu Kwa heshima ya wilaya.
Msanii huyo Mwenye sauti ya kuvutia amemkabidhi Mkuu wa wilaya Cheti cha ushindi pamoja na Keki huku akiahidi kutumia Kipaji chake kuitangaza wilaya ya Babati na Mkoa kwa ujumla ndani na nje ya Tanzania.
Prisca alijishindia kitita cha shilingi Milioni moja na kukabidhiwa na mdhamini wa mashindano hayo Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Manyara Ester Mahawe.
Naye mkuu wa wilaya ya Babati Elizabeth Kitundu amempongeza Prisca kwa Kuwa mshindi wa kwanza kwenye mashindano hayo yaliyowashirikisha washiriki Zaidi ya 500 katika wilaya tano za Mkoa wa Manyara.
Amesema huo ni mwanzo mzuri kwake hivyo aongeze bidii na kujituma pamoja na Kuwa na nidhamu kwenye sanaa hiyo ya mziki ambayo Kwa sasa imekuwa ajira kubwa kwa vijana.
Muandaaji wa mashindano hayo Emanuel Jackson (Imma Entertainment) amesema baada ya mashindano hayo kumalizika ameandaa kitu kingine kinachojulikana kama Gospel Kareoke itakayohusu mziki wa injili ambayo itakuwa ikifanyika Kila jumapili ya mwisho wa mwezi.
Amesema lengo la kuanzisha program hiyo ni kutoa Ajira kwa vijana wenye uwezo wa kuimba nyimbo za aina hiyo haswa wale walioshiriki Manyara Talent search.
Fainali ya Manyara Talent search ilifanyika stendi ya zamani mjini Babati.

No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇