LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 24, 2019

MREMBO KUTOKA MWANZA ATWAA TAJI LA MISS TANZANIA 2019

Miss Tanzania 2019 - 2020 ni Sylvia Sebastian, Huyu ni mrembo kutoka Mwanza ambaye amebadilisha historia yake na kuingia kwenye orodha ya warembo ambao wamewahi kushika taji la Miss Tanzania.

Tukio hilo limefanyika usiku wa kuamkia leo jijini Dar es Salaam.Sylvia ni mhitimu wa kidato cha sita na kwa sasa anasoma kozi ya kompyuta katika Mamlaka ya Elimu ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA).

Mrembo huyo kutoka Mwanza amefanikiwa kupenya katika vipengele vyote ikiwa ni pamoja na uwezo wa kujieleza, ufahamu wa masuala mbalimbali pamoja na jinsi alivyoweza kuutumia uzuri wake wa Kiafrika akiwa jukwaani ndani ya mavazi ya aina tofauti.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe alikuwa mgeni rasmi katika tukio hilo na kushuhudia Sylvia akivishwa taji linalompa nafasi ya kuiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya urimbwende ya dunia (Miss World 2019) yatakayofanyika Desemba 14, London, Uingereza.

Sylvia amepokea taji hilo kutoka kwa Queen Elizabeth Makune aliyekuwa mshindi mwaka 2018.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages