Afisa mmoja mkuu wa serikali amesema kuwa bomu lililolipuliwa na mlipuaji wa kujitoa mhanga katika sherehe ya harusi jana jioni mjini Kabul limesababisha vifo vya mamia ya watu huku wengine wakijeruhiwa.
Kulingana na aliyeshuhudia kisa hicho Gul Mohammad, zaidi ya watu elfu moja walikuwa wamealikwa katika sherehe hiyo huku hofu ikiongezeka kwamba huenda shambulizi hilo likawa baya zaidi kuwahi kutokea mjini Kabul mwaka huu.
Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani ya serikali Nusrat Rahimi, ameliambia shirika la habari la Associated Press kwamba, mshambuliaji alilipua bomu hilo miongoni mwa waliohudhuria harusi hiyo.
Kundi la Taliban na lile linalojiita dola la Kiislamu katika eneo hilo hufanya mashambulizi mabaya katika mji huo mkuu.
Kulingana na Gul, mlipuko ulitokea katika jukwaa ambapo wanamuziki walikuwa wakitumbuiza na vijana, watoto na watu waliokuwa katika eneo hilo waliuwawa.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇