Idara ya Intelijinsia ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imeagiza kufanyika uchunguzi kuhusu matumizi ya serikali ya mpito ya nchi hiyo ambayo imeiongoza nchi kwa muda wa miezi saba sasa tangu kuapishwa Rais wa nchi hiyo, Felix Tshisekedi.
Mkuu wa idara hiyo, Justin Inzun Kakiak amekataa kutoa maelezo juu ya kwa nini ametaka kufanyike uchunguzi kuhusu matumizi ya serikali ya mpito ya Kongo huku jumuiya za kiraia nchini humo zikiituhumu serikali hiyo ya mpito kwa matumizi mabaya ya fedha za umma.
Tangu achukue madaraka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mwezi Januari mwaka huu, Rais FĂ©lix Tshisekedi ameahidi kukomesha ufisadi uliokuwepo katika utawala wa rais aliyemtangulia, Joseph Kabila. Ni vyema kuashiria hapa kuwa, baraza la mawaziri la sasa nchini Kongo lina idadi kubwa ya masalia ya utawala uliopita wa Kabila.
Ufisadi mkubwa umeifanya nchi hiyo kuwa moja ya nchi maskini zaidi duniani licha ya kuwa na utajiri mkubwa wa maliasili za madini kama shaba, cobalt, dhahabu n.k. Ofisi hiyo ya Idara ya Intelijinsia ya Kongo inamuagiza Mkaguzi Mkuu wa Fedha kukagua matumizi yote katika hazina ya serikali ndani ya wizara zote tangu Rais Tshisekedi aingie madarakani. Imeongeza kuwa agizo hilo limetolewa kutokana na sababu za dharura kwa usalama wa nchi.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇