Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. John Pombe Magufuli amemwagiza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kufuatilia malipo yote ya Wagonjwa wanoenda kutibiwa nje ya nchi ili kubaini ubadilifu unaofanywa na baadhi ya watu wasiowaaminifu.
Rais Magufuli ameagiza hilo jana wakati akizindua miradi Saba ya huduma za Afya katika Hospitali ya Rufaa ya kanda ya Ziwa Bugando yenye thamani ya shilingi Bilion15, jambo litalosaidia kurahisisha upatikanaji wa huduma bora kwa ukaribu pamoja na kuokoa kiasi cha fedha miongoni mwa wanaohitaji huduma.
“Na kwasababu Waziri wa Afya yupo hapa, akafuatilie malipo yote ambayo tunatakiwa kulipa, kule nje , akikuta kunamalipo yakulipa mtu ambae hakuwa mgonjwa aliyejihifadhi huko, akazilipe mwenyewe ” alisema Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
Rais Magufuli amesema kuwa baadhiya Watendaji waliona kupeleka Wagonjwa nje ya nchi kwaajili ya matibabu ni fursa yakujipatia kipato, jambo lililokuwa linapelekea hasara kubwa kwa nchi ya Tanzania kutokana na malipo kwa baadhiya watu wasiostaholi.
” Hata kupeleka kwa wagonjwa nje kwa Watanzania ilikuwa ni dili, ilikuwa ni fursa kwa Watendaji, wapo watu waliokuwa wanapewa vibali kwenda kutibiwa India lakini anaumwa mafua, ilikusudi apate safari na msindikizaji, bill zote zinaletwa kwa Serikali ” alisema Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
Dkt. Magufuli aliendelea kusema kuwa ni lazima tujenge nidhamu katika nchi, huku akisisitiza kuwa Serikali haijakataza kupeleka wagonjwa nje ya nchi, huku akisisitiza kuwa wagonjwa wanaostahili kupelekwa kwa matibabu nje ya nchi ni wale walioshindikana ndani ya nchi.
Aidha, ameagiza kuboresha uzalishaji wa oksijeni ili kuhakikisha zinazalishwa kwa wingi jambo litalosaidia kuokoa kiwango kikubwa cha mapato kinachopotea kwa kuagiza nje ya nchi, pia itasaidia kuongeza ajira kwa wananchi wa Tanzania.
“Ninawaomba ndugu zangu, tengenezeni oksijeni nyingi, panueni uzalishaji ili Wizara ya Afya iagize hapa hapa Bugando ili vijana wanaomaliza famasi hapa hapa Bugando wapate ajira hapa yakutengeneza Oksijeni ” alisema Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇