LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 26, 2019

WAZIRI MPINA AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUUAGA MWILI WA AFISA UVUVI UKEREWE.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu wa aliyekuwa Afisa Mfawidhi wa Usimamizi wa Raslimali za Uvuvi kanda ya Ukerewe Ibrahim Jalali katika Hospitali ya Wilaya ya Ukerewe baada ya kushambuliwa na wananchi wakati akitekeleza majukumu yake ya kulinda rasilimali za Taifa kisiwani Siza, kushoto ni Katibu Mkuu Uvuvi Dkt. Rashid Tamatamah.
Wananchi na ndugu wa marehemu wakisikiliza hotuba fupi kutoka kwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina (hayupo pichani) katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe Tarehe 24/07/2019.
Waziri Mpina akitoa salamu na pole kwa familia ya marehemu Ibrahim Jalali nyumbani kwao Rorya Tarehe 25/07/2019.
Waziri Mpina akiwapatia familia ya marehemu Ibrahim Jalali picha yake akiwa anatekeleza majukumu ya kulinda rasilimali za Uvuvi na taifa kwa ujumla (kulia) ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah.
Waziri Mpina akiwa ameshika hati ya ushujaa ya Ibrahim Jalali kwa ajili ya kuwapatia Familia yake juu ya ujasiri na juhidi kubwa aliyoiyonyesha ya   na kupambana na rasilimali za uvuvi Nchini.
Wakazi wa Rorya, Ndugu, Jamaa na Marafiki kutoka maeneo mbali mbali wakiwa wamekusanyika leo  Nyumbani kwa Ibrahim Jalali kwa ajili ya mazishi yake.

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages