Kwa akali watu saba wameuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa kufuatia shambulio la kigaidi dhidi ya hoteli moja kusini mwa Somalia.
Taarifa zaidi zinasema kuwa, waandishi wawili wa habari ni miongoni mwa waliouawa katika shambulio hilo la kigaidi huko katika mji wa Bandari wa Kismayo.
Vyombo vya usalama vinasema kuwa, mlipuaji wa kujitolea muhanga aligongesha gari lililojaa mada za milipuko katika Hoteli ya Asasey katika bandari ya Kismayo kabla ya washambuliaji hao kuvamia jengo hilo.
Mashuhuda wanasema kuwa, walisikia milio ya risasi baada ya bomu lililokuwa ndani ya gari hilo kulipuka. Waziri mmoja wa utawala wa eneo hilo pamoja na wakili ni miongoni mwa waliofariki dunia katika shambulio hilo.
Kundi la kigaidi la wanamgambo wa al-Shabab limetangaza kuwa, wanachama wake ndio waliohusika na shambulio hilo.
Somalia ilitumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 1992 na katika miaka ya hivi hivi karibuni nchi hiyo imeshuhudia kushadidi hujuma za magaidi wa al-Shabab na hivyo kuwasababishia raia wa nchi hiyo matatizo makubwa.
Askari wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika maarufu kama AMISOM wanaokadiriwa kufikia 21,000 wamekuweko nchini Somalia tokea mwaka 2007 ili kujaribu kukabiliana na magaidi wa al-Shabab. Wanajeshi wa Umoja wa Afrika walioko nchini Somalia ni kutoka kkatikka nchi za Uganda, Kenya, Burundi, Somalia, Ethiopia, Djibouti na Sierra Leone.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇