Maafisa kutoka mataifa matatu kusini mwa Asia wamesema leo idadi ya waliokufa kwa mafuriko yaliyotokana na mvua za masika imefikia watu 152 wakati mamilioni ya raia wanakabiliana na hali mbaya iliyosabishwa na mvua zinazoendelea kunyesha.
Takribani watu 90 wamekufa nchini Nepal, 50 katika jimbo la Assam nchini India na wengine kadhaa nchini Bangladesh tangu kuanza kwa mafuriko ya msimu wa masika.
Mamlaka ya kushughulikia majanga kwenye jimbo la Assam nchini India, imesema watu milioni 4.8 katika vijiji 3,700 vilivyopo kwenye jimbo la kaskazini mashariki wameathiriwa na mafuriko.
Katika hatua nyingine, afisa mmoja wa serikali ya jimbo hilo amesema Faru 10 wenye pembe moja, ambao ni miongoni mwa wanyama adimu wamekufa katika hifadhi ya Kaziranga baada ya kingo za mto kupasuka na mafuriko kuingia kwenye mbuga hiyo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇