Waislamu nchini wametakiwa kutekeleza ibada ya hijja kwa kila mmoja mwenye uwezo kwani hija ni nguzo muhimu na ni moja kati ya nguzo tano za Uislamu.
Hayo yameelezwa leo katika Ukumbi wa Sanaa Raha leo Mjini Unguja na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Ayoub Mohammed Mahmoud wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya Mahujaji na Maimamu wa Miskiti Zanzibar yalio andaliwa na jumuiya ya kislamu wa Mashia Tanzania.
Amesema Hija nijambo muhimu kwa kila Muislamu mwenyeuwezo wa hali na mali hivyo ipo haja kutekeleza ibada hiyo ya nguzo ya tano katika Uislam.
Amesema iwapo wenye uwezo wa fedha na kiafya watashindwa kufanya ibada hiyo wajue wanafanya makosa kwani hija ni nguzo inayo mlazimu Muislamu kuitekeleza kwa vitendo.
Hata hivyo alisema Waislamu wanawajibu wa kufanya hija japo mara moja ndani ya umri wake iwapo amejaliwa kuwa na vigezo vinavyo stahiki ikiwemo uwezo, afya na mali.
Aidha alisema Waislamu wafanye hima kuitekeleza kwani Allah akiikubali hija yake na akadumu katika matendo mema mtu huyo malipo yake ni pepo.
“Iwapo Mtu atakubaliwa hija yake na allah na akadumu katika kufanya mema hadi kufa kwake mtu huyo malipo yake ni pepo”alisema Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Ayoub Mohammed Mahmoud.
Akielezea zaidi alisema suala la amani katika nchi ni muhimu hivyo ipo haja ya wananchi kuwamakini kuituza na kuunganisha nguvu zao katika misingi ya dini ili waweze kumtumikia allah kwa wepesi zaidi.
Akizungumzia vitendo vibaya vya uzalilishaji wa watoto na vijana vinavyo favywa na baadhi ya viongozi wa kidini na viongozi wa kitaifa alisema ni jambo moja baya sana kwani linawapotezea heshima utu wao na kuwafanya kutoaminika na jamii.
Alisema wapo baadhi ya watu wanatumiwa vibaya kuiharibu jamii yao kwa udhalilishaji wa kingono, kuwabaka watoto kwa kuwalaghai kwa thamani ndogo isio ya kibinadamu.
Vile vilealisema Mkoa wa Mjini magharibi utachukua hatua kali kwa watu hao bila ya kuoneana haya kwa kufuata sheria na miongozo iliopo.
Nae mwenyekiti wa Jumuiya ya Waislamu wa Shia Tanzania Sheikh Ramadhani Ali Mwelekwa alitoa neno la shukurani kwa Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Ayoub Mohammed Mahmoud na kuomba ushirikiano wa kitaifa pale pakitokea shughuli za kiserikali.
Aidha alisema kuwa Jumuiya yao inatumika kwa kufanya masuala mbali mbali yakiwemo elimu,masuala ya kiafya na maji kwa kutoa huduma kwa jamii ya kitanzania.
Mwenyekiti huyo alimshukuru mkuu wa mkoa kwa kukubali kuungana nao katika mafunzo ya mahujaji na maimamu wa misikiti Zanzibar.

No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇