LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 20, 2019

WANAPOTEZA MUDA WAO WAKIDHANI WANAMZUIA RAIS

Mbunge Nape Nnauye amesema wanaodhani kuwa wanaweza kumkwamisha Rais John Magufuli kugombea urais mwakani wanapoteza muda wao.

Nape ambaye alikuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM amesema kuwa ni utaratibu wa chama hicho kuwa mtu akishapitishwa kugombea awamu ya kwanza, basi ni wazi kuwa atapitishwa kugombea awamu ya pili, na wala jambo hilo halina mjadala.

Amesema kuwa kuna makundi mawali ndani ya chama hicho yanayozungumzia suala la urais 2020. Amesema kundi la kwanzi ni la wageni (wahamiaji au wasiofahamu taratibu) ambao wanadhani kuwa Rais anaweza akazuiwa kugombea awamu ya pili.

Amesema kundi la pili ni lile la wanaofahamu taratibu za chama lakini wameamua kuwa wanafiki kuzungumzia jambo hilo.

Akizungumzia sauti zinazodaiwa kuwa ni yake akizungumza na Abdulrahman Kinana, aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, amesema kuwa jambo hilo lina ujinai ndani yake hivyo, liachwe kwa vyombo husika.
"Kuna kundi ama ni wageni (wahamiaji au hawajui taratibu) ndani ya CCM wanadhani mgombea anayekwenda awamu ya pili anaweza kupingwa, kundi jingine wanajua utaratibu ila wameamua kuwa wanafiki."- Mbunge Nape Nnauye akizungumzia madai ya Rais kuzuiwa kugombea awamu ya pili 2020


Advertisement

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages