LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 24, 2019

VIONGOZI MBALIMBALI WAMPONGEZA WAZIRI MKUU MPYA WA UINGEREZA

Washirika wakubwa wa Uingereza wamempongeza Boris Johnson leo baada ya kushinda uongozi wa chama hicho katika kura ambayo itashuhudia akitawazwa kuwa waziri mkuu mpya wa Uingereza, lakini Umoja wa Ulaya umeonya kuwa kuna nyakati zenye changamoto mbele yao.

Rais wa marekani Donald Trump ameandika katika ukurasa wa Twitter kuwa anampongeza Boris Johnson kwa kuwa waziri mkuu mpya wa Uingereza na atakuwa mtu barabara.

Trump ametangaza kuwa ni shabiki mkubwa wa Johnson. Wiki iliyopita Trump alitabiri kuwa Johnson atatengeneza kile alichokiita maafa ambayo waziri mkuu anayeondoka madarakani Theresa May alizusha wakati akijaribu kuiongoza Uingereza kutoka Umoja wa Ulaya.

Ursula von der Leyen kiongozi anayeingia madarakani kuwa mkuu wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya amempongeza Johnson kwa kusema anatarajia kuwa na uhusiano mzuri nae wa kikazi.

 Wengine waliompongeza Johnson ni pamoja na mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Ulaya wa majadiliano ya kujitoa Uingereza kutoka Umoja huo Michel Barnier , ambaye amesema Umoja huo unataka kufanyakazi na waziri mkuu mpya kuidhinisha makubaliano ya kujitoa na kufanikisha utaratibu mzuri wa Brexit.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages