Ujenzi wa Ofisi na Nyumba za MAAFISA TARAFA Waendelea kushika kasi zaidi huko Newala katika tarafa mbalimbali.
Katibu Tawala wa Wilaya Newala ndg Daniel Zenda akiendelea kusimamia na kufuatilia Ujenzi wa Ofisi na nyumba ya Afisa tarafa katika Tarafa ya Mkunya akiwa na Afisa tarafa wa hapo ndg Lucas Luoga
Amewataka mafundi wa Ujenzi kuendelea kuwa Makini Ujenzi huo kuanzia Ngazi ya Msingi mpaka kukamilisha Ujenzi huo.
Katibu Tawala amejiridhira kiwango kilicho wekwa kwenye BOQ ndicho Fundi alichofanya katika Ujenzi ngazi ya MSINGI, Pamoja na Kufuatilia Agizo alilotoa Mkuu wa Wilaya Mhe Aziza Mangosongo kuwa Mafundi na Vibarua wote Wawena *Vitambulisho Vya Ujasiliamali na Wote wanavyo hivyo agizo limezingatiwa.*
Aidha katibu Tawala ndg Daniel Zenda akipongeza Serikali ya Awamu ya Tanoinayoongozwa na *Mhe Dkt John Pombe Magufuli RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA kwa kuweka Jitihada na Mkakati wa Kuhakikisha kuwafikia Wananchi huko waliko kwa kusogeza huduma za kiserikali katika Maeneo ya karibu kwa KUJENGA OFISI NA NYUMBA ZA MAAFISA TARAFA NCHI NZIMA.
Pamoja na Serikali Kuwapatia *Maafisa Tarafa vyombo Vya Usafiri* kwa Tarafa zote zilizopo Nchi ilikurahisisha na kuongeza tija katika Utoaji wa Huduma kwa Mwananchi na hasa kutatua CHANGAMOTO na KERO za Watanzania kila wakati.
*Tunazidi kuonamafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tano,Pamoja na Wananchi kuzidi kufurahia huduma kwa sasa katika Sekta zote.*
Imetolewa
07/07/2019.
Katibu Tawala Newala.
Your Ad Spot
Jul 9, 2019
Home
Unlabelled
UJENZI WA OFISI NA NYUMBAZA MAAFISA TARAFA NEWALA WAZIDI KUSHIKA KASI
UJENZI WA OFISI NA NYUMBAZA MAAFISA TARAFA NEWALA WAZIDI KUSHIKA KASI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇