Katibu TUGHE Mkoa wa Ilala akizungumza na waandishi wa habari ambapo alianza kwa kumshukuru Mungu na alisema, leo TUGHE Ilala tunafanya Tathmini ya MEI MOSI baada ya kuwatumemaliza kufanya sherehe kwa ujumla pamoja na vyama vingine
Lakini sisi kama TUGHE tukaona ni vizuri kukaa kwa pamoja na kufanya tatmini kwa pamoja ambayo inashirikisha viongozi wa matawi 52 kutoka Taasisi za Serikali na sekta binafsi, lengo ni kuzungumza mambo mbalimbali ya kuboresha Chama pamoja na changamoto zinazo wakabili wafanyakazi
Kwa ujumla mahusiano kati ya TUGHE Mkoa wa Ilala, wanachama, viongozi wa matawi pamoja na mwajiri nimazuri sana, na kwanini nasema nimazuri sana, tunashirikiana kwa pamoja na migogoro sehemu za kazi zimepungua kwa asilimia kubwa sana alisema Mambo.
Pia mfanyakazi anafanya kazi kwa mujibu wa sheria na kanuni na taratibu za kazi na kama pande zote zinazingatiwa migogoro inapungua na huko serikalini mwajiri anatambua vyama vya wafanyakazi
Baada ya Tathmini ya maadalizi ya MEI MOSI ya leo kumalizika ndio maandalizi ya MEI MOSI 2020 ijayo Mungu akijalia akiendelea kutupa kibali cha kuishi alisema mambo.
Mhe, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli alituahidi kabla ya kutoka madarakani atatuongeza mshahara ambapo nikilio kikubwa wa watumishi wa wote Umma na sekta binafsi si kwa TUGHE ni nchi nzima.
Hivyo tunamuombea kwa Mungu ampe maisha marefu na asikie kilio chetu kwani yeye ni msikivu. Mungu azidi kumbariki kwani tunaimani kubwa MEI MOSI 2020 wafanyakzi tutakuwa tunacheka Mambo.
Mwenyekiti TUGHE Taifa, Archie Mntambo akizungumz na waandishi wa abari.
NA KHAMISI MUSSA
Mwenyekiti TUGHE Taifa, Archie Mntambo awataka watumishi wa umma kufanya majukumu yanayo stahili mahala pao pa kazi, nikiwa kiongozi wa Taifa nikwamba watumishi wa umma tunawajibu wa kufanya kazi kwa weledi mkuba
Akizungumza leo July 5, 2019 mara baada ya kuwasili katika kikao cha Tathmini ya MEI MOSI 2019 cha viongozi wa matawi Mkoa wa Ilala Dar es Salaam kilichofanyika Ukumbi wa Mgulani JKT
Alisema tumepata bahati ya nafasi ya kuwa na mkuu wa nchi ambaye anatujali na sisi tuonyeshe dhamira yetu kwa kufanya kazi kwa bidii kuhakikisha Tanzania nikati ya nchi imepiga mafanikio makubwa katika maendeleo ya uchumi na maendeleo ya wananchi wake
Katika sekta mbalimbali lakini sisi tukihusika katika sekta ya afya na sekta ya serikali kuu, tukiwa na dhamana kubwa katika nchi hii kuliko vyama vyote vya wafanyakazi, sisi ndio tunatoa taswira ya serikali tuliyonayo na tunato taswira ya utumishi uliotukuka.
Mwenyekiti Tawi la TUGHE, Hospitali ya Hindumandari, Ibrahim Mbaga akizungumza na viongozi wa matawi alisema, namshukuru mgeni rasmi kwa kukubari mwaliko wetu na Mungu atuzidishie umri mrefu alisema Mbaga.
Pia niseme kwamba tumepata mwenyekiti anayefanya kazi za TUGHE, sisi kama wanachama tunaamini TUGHE ni Taasisi na TUGHE ndio Tanzania.
Mwenyekiti nikuhakikishie leo matawi yoliopo hapa ni 22 pamoja na kuwepo Sherehe za Sabasaba hivyo Tughe Dar es Salaam Ilala ndio TUGHE Taifa na tukilala sisi ujuwe Tughe nzima imelala.
Tunakushukuru kwa kututia moyo na tuendelee kuongeza wanachama, kipekee niendelee nikupongeze kwa kutoa maagizo kwa viongozi wa Mkoa na Wilaya kwa lengo la kuvuna wanachama elfu moja na miatano. Pongezi kwako ila kwa maelekezo yako ndio haya yamefanyika vizuri.
Hotuma yako tumeipokea na sisi tunachukulia kama mpango kazi na haya ni maagizo kutoka ngazi za juu tutayafanyia kazi na sisi kama viongoazi wa matawi tunalo jukumu ya kuyatekeleza kama haya ni maagizo ya Mwenyekiti wa Taifa na Mungu atatusaidia tuyafanyie kazi vizuri.
Lakini Mwenyekiti sisi kama viongozi wa matawi pia niombe kwa niaba ya wenzangu niseme kuwa umetuona tumechangamka ni kwa sababu ofisi ya Mkoa Ilala imechangamka na tupa vizuri na hamasa ni kubwa na ndio maana baadhi ya wafanyakazi wangi wameanza kuijuwa TUGHE wanafikiri TUGHE ndio TUCTA.
Hata wa vyama vingine wanapenda wapate taarifa zao kupitia Tughe hili nakuhakikishia na tunachoomba kutoka kwako ni kupiti ofisi yako ihakikishe sekta binafsi bado inachangamoto nyingi.
Tunaiomba ofisi yako ihakikishe kwamba katika TUGHE kuna sekta binafsi na kunachangamoto nyingi aina hiyo bapo katika TUGHE kuna sekta binafsi ambapo kuma kuna Hospitali binafsi na nyingine tutie harakati na sekta binafsi ziingie
Tunataka Mwenyekiti wetu akisema neno na Serikali ijuwe wafanyakazi wamesema wanataka nini, milioni 205 na kuendelea hii nikama motisha kama zawadi wamepewa lakini tunaomba tamkolingine litoke kuwa zawadi nyingine ziongezwe ili wapate zawadi watakazo zikumbuka wao na vizazi vyao
Bodi za mishahara hazikuwajubika kwa kipindi hiki na kuna wastaafu wengine hakizao hawajapata, pia nikushukuru kwa wewe kutoa ruhusa za mkutano kule Mtwara tulifaidika na mafunzo kwa aina hii ziendelee kufanyika kila mwaka na chachu ndani ya chama chetu itaongezeka.Mwenyekiti niseme haya kwa kukupongeza kwa uchapakzi wako na kushirikiana na viongozi wako asanteni sana kwa kunisikiliza na Mungu awabariki
Meneja wa Kanda ya Mashariki wa Sanlam Life Insurance, Abihadi Ikimbia akizungumza jambo katika Mkutano wa Tathmini jinsi wanavyotoa huduma mara baada ya kuzungumza Mgeni rasmi |
Naibu Katibu TUGHE , Jane Mbulla akizungumza jambo wakati wa Mkutano wa Tathmini ya MEI MOSI uliofanyika Ukumbi wa Mgulani JKT alisema; nawashukuru kwa kupanga wenyewe na kuja kufanyatathmini katika kila kazi
Kunakujitathmini kwa hiyo tumeamua kujithmini na kukutana na kuzungumza na hata kujikosoa na kubadilishana mawazo na huyo mzowefu kwamba katika Tawi lako mwenzangu unafanyaje, kuna nini na kunachangamoto gani unazokutana nazo, katika swala hili lililotufanya tukutane hapa tathimini ya MEI MOSI nakazi za Chama Mkoani niwapi mimi
nimeshindwa pengine na kutiana moyo kwa hiyo nimependa naomba niwashukuru sana.
Lakini kunajambo moja Mhe, Mgeni rasmi kabla sijakutambulisha iliuzungumze na viongozi hawa wa matawi katika matawi nimesikia kunamatawi ambayo baadhi ya matawi ya kamati ya wanawake hazipo maana ya matawi
Nimekuwa nikipitia taarifa yako ya 52 lakini kamati za wanawake zipo 40 nilikuwa natamani viongozi wa matawi na viongozi wa viongozi wa kamati za wanawake pengine na katibu kwa ujumla hili nalo tuliangali iliwende sawa.
Kwanamna hiyo niwapongeze kwa kazi njema mnayoifanya kwa ushirikiano mnao uonyesha na kwa ushirikino na Katibu wa Mkoa na kazi za chama. Chama kipo hai Mkoa wa Ilala.
Baada ya maelezo hayo mafupi nipende kumtambulisha, Mwenyekiti Taifa TUGHE , Mr. Archie Mntambo ambaye ni mgeni rasmi katika hafla hii ya Mkutano wa tathmini
Mwenyekiti Kamati ya Wanawake Tawi la TUGHE MOI na Afisa Muuguzi wa Taasisi hiyo Georgina Chirwa akisoma taarifa za kazi za chama kuanzia Apr 2018 na Juni 2019 kwa Viongozi wa Matawi Mkoa wa Ilala kwa Mwenyekiti TUGHE Taifa
viongozi wakipunga mikono kwa ishara ya kumpongeza Katibu wa TUGHE Mkoa wa Ilala Tabu Mambo kwa utendaji wake wa kazi na kushirikisha mambo mbalimbali ya chama kwa kuweka wazi |
Mwenyekiti TUGHE Taifa, Archie Mntambo (watatu kulia) walio kaa akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa matawi Mkoa wa Dar es Salaam July 5, 2019 katik Ukumbi wa Mgulani JKT
Mwenyekiti TUGHE Taifa, Archie Mntambo akizungumza na viongozi wa matawi mbalimbli katika Ukumbi wa Mgulani
Kaimu Mwenyekiti TUGHE Mkoa na Mjumbe Kamati ya Utendaji ya Dar es Salaam Dkt. Peter Kibacha akizungumza jambo wakati alipokuwa akifungua Mkutano huo, kuanzia kulia ni mdhamini Joyce Chirwa, Katibu TUGHE Mkoa wa Ilala Tabu Mambo na Mwenyekiti TUGHE Taifa, Archie Mntambo
Mwenyekiti TUGHE Taifa, Archie Mntambo (kulia) akizungumza jambo na viongozi mbalimbali wa Chama hicho wakati wa Mkutano wa Tathmini ya MEI MOSI 2019
Tatibu TUGHE Mkoa wa Ilala Tabu Mambo akitoa utambulisho mfupi
Baadhi ya viongozi wakipiga makofi wakati Mwenyekiti TUGHE Taifa, Archie Mntambo alipo wasili Katika Ukumbi wa Mgulani JKT
Kaimu Mwenyekiti Mkoa na Mjumbe Kamati ya Utendaji Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Peter Kibacha kielekeza jambo kwa mmoja wa viongozi kutoka Tawi la TUGHE la Jeshi la Polisi
Baadhi ya viongozi wakimsikiliza Mwenyekiti TUGHE Taifa, Archie Mntambo alipokuwa akizungumza katika Mkutano wa Tathmini ya MEI MOSI 2019
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇