LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 15, 2019

RC ZAMBI AWAASA WASTAAFU KUWA NA MAADILI


Na Ahmad Mmow-Lindi

Mkuu wa mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi amewaasa wastahafu mkoani humu wazingatie maadili mema baada ya kumaliza utumishi wa umma.

RC Zambi alitoa rai hiyo wakati wa hafla ya kuwaaga wastafu wa Jeshi la Polisi na kuwakaribisha askari wengine waliohamishiwa mkoani humu.

Hafla ambayo ilifanyika jana katika mjini  Lindi, Mkuu huyo wa mkoa wa Lindi ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Lindi, alisema wastahafu wawe wa adilifu wanapoanza maisha mapya uraiani.

Alibanisha kwamba baadhi ya askari, wakiwamo maofisa baada ya kustahafu wamekuwa wakijiingiza kwenye makundi ya kihalifu. Kitendo ambacho ni kibaya ambacho hakistahili kufanywa na askari hao wastahafu ambao walipokuwa katika utumishi wa umma walikemea na kupambana kukomesha vitendo hivyo.

"Baadhi ya askari baada ya kustahafu utumishi wa umma wanajiingiza kwenye  ujambazi na vitendo vingine visivyokubalika kwa mujibu wa sheria,'' alisema Zambi.

Mbali na hayo, Mkuu huyo wa mkoa alitoa wito kwa watumishi waliobado kazini kujiandaa katika maisha ya ustahafu ili watakapo maliza muda wao wa utumishi wasijiingize katika uhalifu kutokana na ugumu wa maisha.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages