NA SALVATORY NTANDU
Mkazi wa kijiji cha Bugoshi,kata ya Uyogo halmashauri ya Ushetu Daudi Bundala anatafutwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma ya kumua dada yake Suzana Bundala(21) kwa kumpiga kitu kizito kichwani na kumsababishia kifo,baada ya kumkuta akiwa amelala na mpenzi wake nyumbani kwao.
Kamanda wa polisi mkoa shinyanga (ACP) Richard Abwao amethibitisha kutokea kwa tukio hilo nakusema tukio hilo lilitokea julai 12 mwaka huu saa tano usiku katika kijiji cha Bugoshi,kata ya Uyogo tarafa ya Mweli wilaya ya kipolisi Ushetu.
Amesema, chanzo cha tukio hilo ni marehemu kukutwa akiwa na mpenzi wake aliyefahamika kwa jina la Eddy Nkimbila nyumbani kwao kitendo kilichomchukiza Daudi na kumshambulia dada yake na kumsababishia kifo.
Amefafanua kuwa baada ya kumshambulia dada yake na kumsababishia kifo Daudi alikimbia mara baada ya tukio hilo na juhudi za kumtafuta na kumkamata zinaendelea nakuongeza mwili wa marehemu umekabidhiwa kwa ndugu zake kwa taratibu za mazishi.
Hata hivyo Kamanda Abwao ametoa wito kwa wananchi Mkoani Shinyanga kuacha mara moja tabia ya kuendelea kujichukulia sheria mkononi na kufikia maamuzi ya kufanya matukio vya kikatili ambayo yanaweza kusababisha wakachukuliwa hatua za kisheria.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇