LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 16, 2019

RAIS MAGUFULI MGENI RASMI MAADHIMISHO MIAKA 80 YA TAG


Na Ferdinand Shayo,Arusha.

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha Maadhimisho ya miaka 80 tangu kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG)  limeanzishwa nchini Tanzania ambapo maelfu ya waumini watakusanyika katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha .

Askofu Mkuu wa Kanisa hilo Dr.Barnabas Mtokambali akizungumza na Wanahabari jijini hapa amesema kuwa maadhimisho hayo yanafanyika kitaifa jijini Arusha ambapo kilele chake ni Julai 21 mwaka huu ambapo viongozi mbalimbali watahudhuria wakiwemo viongozi wa serikali wakiongozwa na Rais Magufuli.

Dr.Barnabas amesema kuwa maadhimisho hayo yanaambatana na mkutano mkubwa wa injili,huduma ya upimaji macho na matibabu ,uzinduzi wa visima vya maji pamoja na kutoa vifaa vya shule katika shule tano za jiji la Arusha.

Pia amewataka wakazi wa Arusha kuhudhuria katika mkutano huo mkubwa utakaowaleta watu wote pamoja na kuwa na Waimbaji wakubwa wa nyimbo za Injili akiwemo Miriam Mauki na Julia Wilkander .

Alisema pia Muhubiri wa kimataifa Johannes Amritez atakuwepo kwa siku zote za mkutano huo pamoja wahubiri kutoka ndani ya nchi.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages