LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 15, 2019

POLEPOLE AWEZESHA KIJANA MLEMAVU WA MACHO KUPATA ADA YA KUSOMA SHAHADA


Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi  (CCM) Taifa,Humphrey Polepole,Akimpongeza Mhitimu wa Elimu ya Stashahada kutoka Chuo cha Adem,Justin Milanzi (Wa Pili kutoka Kulia) Baada ya Kuwasilisha Changamoto Zake za Kuomba Kusaidiwa Udhamini wa Ada ya Masomo ya Elimu ya Juu (Shahada) kwa Njia ya Uimbaji katika Mahafali ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Pwani Yaliyofanyika Wilayani Bagamoyo katika Ukumbi wa Tasuba leo.Picha Zote na Elisa Shunda
 
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi  (CCM) Taifa,Humphrey Polepole (Katikati) Akizungumza katika Mahafali ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Pwani Yaliyofanyika Wilayani Bagamoyo katika Ukumbi wa Tasuba leo. Kulia Kwake ni Mwenyekiti wa Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Pwani,Phillemon Mabuga,Mwenyekiti wa UVCCM Pwani,Charangwa Makwiro na Katibu wa CCM wa Mkoa Huo,Ally Makoa. 

 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi  (CCM) Taifa,Humphrey Polepole (Katikati) Akiongoza Maandamano Kuelekea Chuo cha Taasisi Sanaa na Utamaduni Bagamoyo kwa Ajili ya Mahafali ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Pwani Yaliyofanyika Wilayani Bagamoyo katika Ukumbi wa Tasuba leo.


Wahitimu wa Vyuo na Vyuo Vikuu wa Ngazi ya Cheti na Diploma kutoka Vyuo Mbalimbali kwa Mkoa wa Pwani wakifuatilia kwa Makini Wakati Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Humphrey Polepole (hayupo Pichani) Akizungumza katika katika Mahafali ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Pwani Yaliyofanyika Wilayani Bagamoyo katika Ukumbi wa Tasuba leo.


Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini,Slyvestry Koka (katikati) Akizungumza katika Mahafali Hayo.


NA:ELISA SHUNDA,BAGAMOYO,PWANI.

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Humphrey Polepole Amewezesha Kijana Justin Aliyehitimu Elimu ya Stashahada katika Chuo cha Adem Kupata Ada ya Kumuwezesha Kusoma Elimu ya Shahada katika Chuo Kikuu cha Dododma kutokana na Michango Mbalimbali Iliyotolewa na Baadhi ya Wabunge na Viongozi Waliokuwepo katika Mahafali ya Vyuo na Vyuo Vikuu kwa Mkoa wa Pwani Vilivyofanyika Tasuba Bagamoyo Leo Ambapo Zaidi ya Vijana 200 Makada wa Chama Hicho kutoka Vyuo vya Mkoa wa Pwani Walihitimu.

Akizungumza katika Mahafali hayo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Humphrey Polepole aliwapongeza Wanachuo Hao kwa Kuhitimu Elimu Zao na Kutoa Rai kwa Vijana Hao Wasomi Ambao ni Makada wa CCM Kutumia Elimu Waliyopata katika Kuhakikisha Wanakwenda Mtaani Kuzungumza na Vijana Wenzao Kuwaelezea Miradi Mikubwa ya Kimaendeleo Inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)  Inayosimamiwa na Mwenyekiti Wake na Rais Dk.John Magufuli.

“Kwanza Nawapongeza Sana kwa Kuhitimu Masomo Yenu Sasa Mnakwenda Mtaani Ombi Langu Kwenu Mkiwa Kama Vijana Wasomi Ambao ni Makada wa CCM Mkaisemee Mema Serikali Yenu iliyo Chini ya CCM kwa Yale Inayotekeleza Ipo Miradi Mikubwa Inaendelea Kujenga Ujenzi wa Bwawa Kubwa la Umeme Afrika Mashariki (Stigle Gorge),Ujenzi wa Reli ya Mwendo Kasi (SGR),Ujenzi wa Barabara za Juu (Fly Over),Upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere,Ufufuaji wa Shirika la Ndege Nchini kwa Kununua Ndege Nane za Kufanyia Biashara ya Kubebea Abiria na Kupeperusha Twiga Twiga Wetu;

“ Nyie Wenyewe Mnajua Wenzetu Upande wa Pili Hawatusemei Mema Hivyo Ninyi Mkiwa Kama Vijana Wasomi Sasa Mkazungumze na Vijana Wenzenu na Jamii Inayowazunguka Kuhusu Yale Yanayotekelezwa na Serikali Yao Wasisikilize Uongo wa Wenzetu wa Upande wa Pili Wanayosema Kuwa Serikali ya Awamu ya Tano Haijafanya Kitu ni Waongo Wakubwa,Niseme Tembeeni Kifua Mbele Mkiweka Imani kwa Rais wetu Magufuli na Uongozi Wake kwa Hakika Wanachapa Kazi Sana” Alisema Polepole.

Aidha katika Mahafali Hayo Mmoja Kati ya Wahitimu wa Stashahada ya Elimu kutoka Chuo cha Adem Ambaye ni Mlemavu wa Macho,Justin Milanzi aliweza kuchangiwa Ada ya Kuendelea na Masomo ya Elimu ya Juu (Shahada) katika Chuo Kikuu cha Dodoma kwa Kuwasilisha Changamoto Yake ya Maisha Kupitia Sanaa ya Uimbaji,Ambapo Viongozi Waliokuwepo Walihamasika Kujitolea Kumchangia Ada ya Miaka Mitatu na Nauli ya Kusafiri Kuelekea Mkoani Dodoma Kufuatilia Mchakato wa Kuanza Masomo Yake.

Katika Mchango Huo wa Kumuwezesha Mhitimu Milanzi Kuendelea na Elimu ya Juu,Mbunge wa Kibaha Mjini,Slvestry Koka,aliahidi kumlipia Mwaka wa Kwanza wa Masomo Yake Pamoja na Kutoa Shilingi Milioni Mbili kwa Ajili ya Kurekodi Nyimbo za Kukinadi Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Chaguzi Zijazo za Serikali ya Mtaa na Uchaguzi Mkuu,Mbunge wa Bagamoyo,Dk.Shukuru Kawambwa, Aliahidi Kumsomesha Mwaka wa Pili, Mke wa Mbunge wa Kibaha Mjini,Mama Celina Koka,Aliahidi Kumlipia Mwaka wa Tatu,Mkuu wa Chuo cha Tasuba,Dk.Sixten Masanja Aliahidi kumpatia Sh.500,000,Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani,Ramadhan Maneno Aliahidi Kuchangia Shilingi Laki Moja.  

Pia Mwenyekiti wa Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Pwani,Phillemon Mabuga,Aliwasihi Vijana Hao Kuwa Wavumilivu kwa Kuwa Wanakwenda Mtaani Watakutana na Changamoto za Ajira Ila Hawapaswi Kukata Tamaa Wanapaswa Kutumia Elimu Waliyopata katika Kubuni Miradi Mbalimbali Lakini Uvumilivu Uwe Nguzo Yao kwa Kuwa Hata Yeye katika Maisha ya CCM Aligombea Nafasi Nyingi Bila ya Mafanikio Lakini Bado Hakati Tamaa Hadi Sasa Bado Anakitumikia Chama Hicho kwa Uaminifu.

Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani (UVCCM),Charangwa Makwiro, Aliwasisitiza na Kuwakumbusha Vijana Hao Wasomi Makada wa Chama Hicho Kujitokeza Kuchukua Fomu za Kugombea Uongozi wa Serikali za Mitaa Unaotarajiwa Kufanyika Novemba Mwaka Huu na Uchaguzi Mkuu wa Mwakani katika Nafasi ya Udiwani na Ubunge na Kuwaambia UVCCM Mkoa Huo Itakuwa Pamoja Nao katika Kuwasapoti na Kuwasemea.

Kwa Upande Wake Mratibu wa Shirikisho la Walimu Taifa,Mwalimu Joyce Francis Aliwapongeza Vijana Hao Wahitimu kwa Kumaliza Elimu Yao kwa Ngazi ya Astashahada na Stashahada na Kuwasihi Kutumia Elimu Waliyopata katika Kujitengenezea Ajira Binafsi Itakayoifanya Jamii Inayowazunguka Kutambua na Kuthamini Elimu Waliyonayo na Muda Waliotumia Pindi Wakiwa Chuoni.

Mwishoooo

0719976633.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages