LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 13, 2019

RAIS MAGUFULI AMSHUKURU MUSEVENI

Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemshukuru Rais Museveni kwa kuhakikisha afanya msaada wa Mama Maria Nyerere kuhakikisha anapata matibabu kwa haraka baada ya mama huyo kuugua ghafla.

Rais Magufuli amemshukuru pia kwa kutoa ndege ya Uganda Airline ikamleta hadi Dar es salaam kwaajili ya mama huyo kupatiwa matibabu.

''Tunakushukuru Mh. Museveni, mwezi Juni 2019, Mjane wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere, aliugua ghafla akiwa nchini Uganda na ulihakikisha anapata matibabu kwa haraka na ukatoa ndege ya Uganda Airline ikamleta hadi Dar es salaam'', amesema Rais Magufuli leo akiwa Chato Mkoani Geita.

Aidha Rais Magufuli amesema"Asante sana Rais Museveni, kwenye tetemeko la Bukoba ulitusaidia kwenye  Mv Nyerere ulikuwa wa kwanza pia, hii inaonyesha ni namna gani umekuwa ndugu yetu."

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages