LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 4, 2019

PROF. KUTOGOMBEA UBUNGE TENA

Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka (CCM), amesema hatagombea tena nafasi ya ubunge Uchaguzi Mkuu ujao.

Profesa Tibaijuka aliyepata kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakati wa Serikali ya awamu ya nne, alitoa kauli hiyo wakati akihojiwa na mtandao wa Millard Ayo.

Pamoja na mambo mengine, alisema anastaafu kwa sababu yeye ni kizazi cha Mwalimu Julius Nyerere ambaye aliwafundisha kung’atuka.

“Mimi 2020 ninastaafu, ninang’atuka kwasababu sisi ni kizazi cha Mwalimu Nyerere na katika vitu alivyotufundisha ni kung’atuka.

“Katika uchaguzi wa 2015, Muleba Kusini pamoja na kampeni ya Escrow bado nilipita kidedea, kwa kweli nawashukuru wananchi wa Muleba, ni watu wanaotafuta maendeleo, wana kiu ya maendeleo.

“Na ninaposema nastaafu ubunge, haimaanishi kwamba nastaafu Muleba, hivi ni vitu viwili tofauti, mimi ninastaafu uwakilishi, Bunge letu hili lingekuwa Seneti ningesema nitaendelea.

“Lakini sasa ni Bunge la Uwakilishi, hatuna Bunge la Seneti, yaani Bunge ambalo sasa hoja zinalinda masilahi mapana ya umma, hapa tunawakilisha wananchi na mimi naamini tunaweza kupata mwakilishi mzuri wa Muleba,” alisema.

Mwanasiasa huyo ambaye pia aliwahi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), alisema sasa anarudi kwenye jamii akiwa kama mwanaharakati.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages