LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 12, 2019

NDEGE YATUA KWA DHARURA

Ndege ya shirika la ndege la Air Canada iliyokuwa ikielekea Australia siku ya jana ililazimika kutua kwa dharura mjini Hawaii huku abiria 37 ikiwa ni pamoja na wafanyakazi wa ndege hiyo wakijeruhiwa baada ya kupigwa na dhoruba ya ghafla.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na msemaji wa Air Canada Peter Fitzpatrick, ndege hiyo ya aina ya Boeing 777-200 ilikuwa imebeba abiria 269 na wafanyakazi wa ndege 15 safari kutoka Vancouver hadi Sydney.

Abiria wamesema dhoruba hiyo iliwarusha watu hewani, baadhi wakigonga paa la ndege. Wengi walielezea kuwa lilikuwa ni tukio la kuogofya sana.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages