LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 14, 2019

MTATIRO AZUNGUMZA BAADA YA KUTEULIWA NA RAIS MAGUFULI

Mapema hii leo Rais John Magufuli alimteua kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tunduru aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Chama Cha wananchi (CUF) Julius Mtatiro, ambaye alitangaza kuhamia CCM mwaka jana.

Kabla ya Mtatiro kushika nafasi hiyo, awali ilikuwa ikishikiliwa na Juma Homera ambaye kwa sasa ameteuliwa kuwa  Mkuu wa Mkoa wa Katavi.

Akizungumzia uteuzi huo, Julius Mtatiro amesema kuwa amezipokea taarifa hizo akiwa safarini na pia amezipokea kwa mshtuko sana.

"Kwa sababu sikutarajia kwamba naweza kuteuliwa na Rais, unajua ukiteuliwa halafu hukuwa unatarajia unapata mshtuko sana." ameeeleza.

Ameendelea kwa kusema, "Ila ukimaliza kupokea kwa mshtuko hizo taarifa inabidi ukubaliane nazo tu, kwa sababu ni kazi ya umma na hakuna budi kuitumikia".

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages