Waziri wa Utalii na maliasili nchini Tanzania Dkt. Hamis Kigwangalla ameelezea kuguswa na vifo vya watu waliofariki katika jali hii leo.
Watano wakiwa ni wafanyakazi wa Azam Media ambapo wamepata ajali ya gari iliyotokea kati ya Shelui na Igunga. Wawili wapo mahututi, mmoja hali yake si mbaya.
"Moyo wangu umeshtuka na unatoa machozi ya damu kupata taarifa za kushtua na kusikitisha za ajali ya wafanyakazi wa Azam Media iliyotokea maeneo ya Malendi, Singida na kuchukua maisha ya 7 kati ya 10 waliokuwepo. Tunahangaika kutafuta usafiri wa haraka wa majeruhi hao 3," ameeleza Waziri Kigwangalla
Ajali hiyo imetokea wakiwa njiani kuelekea Chato kwa ajili ya kwenda kuonesha shughuli ya TANAPA ambapo mgeni rasmi alitarajiwa kuwa Rais John Magufuli

No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇