LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 12, 2019

KAMISHNA MHIFADHI WA MISITU AWASILI MAKAO MAKUU YA TFS DAR

Kwa mara ya kwanza tangu avishwe cheo cha Kamishna Mhifadhi wa Misitu na Dkt Hamisi Kigwangalla, Waziri wa Maliasili na Utalii na hatimaye kula Kiapo cha Utii na uadilifu mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli Julai 9, 2019, Kamishna Prof. Dos Santos Silayo amewasili makao Makuu ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Jengo la Mpingo jijini Dar es salaam na kupokelewa na Viongozi Waandamizi na watumishi wa TFS.

Akizungumza na watumishi wake mara baada ya kuwasili ofisini hapo, Kamishna Prof. Silayo alisema mabadiliko yanayotokea katika sekta ya maliasili yamepelekea pia kubadili mfumo wa usimamizi na utendaji wetu toka ule wa Kiraia kwenda Jeshi Usu. “Namshukuru Mungu kuwa sehemu ya mabadiliko hayo. Hatua hiyo ikapelekea kuvishwa cheo cha Kamishna Mhifadhi wa Misitu na Mhe Dkt. Hamisi Kigwangalla, Waziri wa Maliasili na Utalii na kula Kiapo cha Utii mbele ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Dkt. John Pombe Magufuli siku ya tarehe 9 Julai 2019.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages