LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 19, 2019

BILIONI 600 KUMALIZA CHANGAMOTO YA USAFIRI KIGOMA.

Na Rhoda Ezekiel Kigoma,

Serikali ya Tanzania na Burundi zimetambulisha miradi ya ujenzi wa barabara kutoka Kabingo na Manyovu yenye urefu wa kilomita 260.6 huku Burundi ikizindua Barabara ya Rumonge na Gitaza yenye kilomita 45 ili kurahisisha huduma ya usafiri na kuchochea uchumi kwa kufungua biashara  kwa Nchi hizo.

 AKizungumza wakati wa uzinduzi wa kongamano la kuzindua  mradi huo lililofanyika jana Mkoani Kigoma ,Naibu waziri wa Ujenzi na Uchukuzi  mhandisi Atashasta Nditiye  alisema Serikali imetenga zaidi ya shilingi bilioni 600 kwaajili ya kukamilisha mradi huo na kuwahakikishia Wananchi wa Kigoma Changamoto ya usafiri kumalizika.


Alisema changamoto kubwa ya Mkoa wa Kigoma ni kutokuwa na barabara za lami zinazo waunganisha na mikoa mingine na Nchi zingine lakini Rais baada ya kuliona hilo ameamua kuwekeza fedha hizo katika barabara ilikufungua fursa za kiuchumi katika Mkoa huo.


"Natambua ya kuwa tunaelekea katika uchumi wa viwanda zipo bidhaa nyingi zitakuwa zikisafirishwa kwendwa kuuzwa Nchi mbalimbali, kigoma ni mkoa ambao unaungana na Nchi tatu za Burundi, Rwanda na Congo Barabara hii ikikamilika itakuwa ni Chachu kubwa kwa Watanzania na Warundi kufanya biashara  kwa pamoja na  itajenga mahusiano mazuri",

Aidha Nditiye alimshukuru Rais kwa kuukumbuka mkoa wa Kigoma kwa kufanya mahusiano Mazuri na Rais wa Burundi kuhakikisha Barabara hizo zinajengwa na kuwataka Wananchi kutumia  fursa hiyo kwa kujikwamua na umasikini. 


Nae mtendaji Mkuu wa wakala wa Barabara Tanzania (TANROAD) Mhandisi Patrick Mfugale alisema mradi huo unaoanza mwezi wa nane utakuwa kichocheo cha uchumi kwa nchi ya Burundi na Tanzania kupitia masoko ya ujirani mwema hivyo kukuza uchumi wa Wananchi.

Alisema changamoto kubwa ya Mkoa wa Kigoma na Nchi ya Burundi, ni kutokuwepo na Barabara, hali inayopelekea kuwepo na ugumu katika usafirishaji wa mazao, serikali kwa kulitambua hilo imetenga fedha kwaajili ya kukamilisha ujenzi wa Barabara hiyo na kuweza kufungua fursa za kibiashara.


Mkuu wa mkoa wa Kigoma Brigedia General Mstaafu Emmanueli Maganga alisema mkoa huo, ndio pekee Tanzania ambao haujaungwa na mikoa mingine pamoja na kumuagiza mhandisi wa TANROAD Mkoa wa Kigoma kuzingatia kanuni za ujenzi wa barabara kuepusha adha kwa watumiaji na wananchi. 

Pia aliwataka Wananchi wa Kigoma kuchangamkia fursa wakati wa ujenzi wa Barabara hizo, kuhakikisha wanapata nafasi za kuwa vibarua ilikuweza kujiingizia kipato na kuomba mradi huo ukamilike kwa wakati iliwananchi waanze kutumia fursa hizo.

Alisema Wananchi wa kigoma Wanaona nao wanakumbukwa kutokana na miradi mbali mbali  na kuhakikisha mkoa wa Kigoma unainuka kiuchumi na kuendelea katika maendeleo.

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages