LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 16, 2019

BARAZA LA HAKI ZA BINADAMU LA UMOJA WA MATAIFA LALAANI VIKWAZO VYA MAREKANI DHIDI YA NCHI MBALIMBLI

Marekani imekuwa ikitumia fimbo vya vikwazo dhidi ya nchi mbalimbali duniani kwa ajili ya kufikia malengo yake ya kijuba na kimabavu.
Kwa sababu hiyo, Jumatatu ya jana tarehe 15 Julai Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa lilipasisha azimio linalolaani vikwazo vya Marekani. Muswada wa azimio hilo ulipendekezwa na Venezuela na Palestina kwa niaba ya nchi wanachama katika Jumuiya ya Nchi Zisizofungamana an Upande Wowote (NAM). Baada ya kupasishwa azimio hilo, Rais Nicolás Maduro wa Venezuela amezishukuru nchi wanachama katika Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa na kusema: "Azimio hili ni ushindi unaoimarisha ushirikiano wa kimataifa na kuzima athari za vikwazo vya tawala za kibeberu."
Nicolás Maduro
Japokuwa vikwazo vya Marekani vimekuwa vikiwekwa dhidi ya nchi nyingine hususan wapinzani wa sera za kibabe za Washington kwa visingizio mbalimbali vya kisiasa, kiuchumi, kiusalama na haki kwa madai ya haki za binadamu, lakini sababu halisi ya hatua hiyo ni kutaka kutimiza malengo na maslahi ya Marekani. Serikali ya Donald Trump inaamini kuwa, mashinikizo hususan ya vikwazo ndio wenzo bora zaidi wa kufikia malengo yake katika nchi nyingine. Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Aaron Wess Mitchell anasema: Vikwazo ni wenzo wa kistratijia, na kwa sasa Marekani imeweka vikwazo 4190 katika maeneo mbalimbali ya dunia. Vikwazo vya Marekani dhidi ya nchi nyingine katika kipindi cha utawala wa Donald Trump vinatekelezwa zaidi kwa shabaha ya kuziondoa madarakani tawala za nchi hizo, kuwapiku washindani wa kibiashara na kuhodhi makoso ya kiuchumi.
Mwezi Mei mwaka huu wa 2019 ripota maalumu wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, Idriss Jazairi alisema: "Vikwazo vya kiuchumi vya Marekani dhidi ya nchi za Cuba, Venezuela na Iran vyenye malengo ya kisiasa ni ukiukaji wa haki za binadamu na sheria za kimataifa." Serikali ya Trump imekuwa ikitumia vikwazo hivyo kama wenzo wa mashinikizo ya kutaka kuziondoa madarakani serikali za nchi hizo. Mbali na kusitisha mchakato ulioanzishwa na Barack Obama wa kuboresha uhusiano na Cuba, Donald Trump alianza teka kutekeleza vikwazo dhidi ya nchi hiyo. 
Donald Trump
Kuhusiana na Venezuela pia tangu mwaka 2017 serikali ya Washington imewawekea vikwazo maafisa 150 wa taasisi mbalimbali za nchi hiyo na inafanya mikakati ya kuilemaza kiuchumi na kifedha serikali ya Caracas. Pamoja na hayo vikwazo vikubwa zaidi vya Marekani vimeelekwa kwa Iran. Baada ya kuiondoa Marekani katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA, mwezi Mei mwaka 2018 Donald Trump alianza kutekeleza vikwazo ambavyo havijawahi kushuhudiwa dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu. Vikwazo hivyo vinajumuisha sekta ya mafuta. Kiongozi huyo mbaguzi ametishia kwamba atazidisha vikwazo hivyo.
Kwa kutilia maanani athari mbaya za vikwazo vya upande mmoja vya Marekani kwa nchi nyingine, nchi zote zimekuwa zikikosoa sera hiyo ya mabavu na kusisitiza udharura wa kukabiliana nayo hasa kwa kutilia maanani kwamba, vikwazo hivyo vinatekelezwa bila ya idhini ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Vilevile nchi hizo zinasisitiza udharura wa Marekani kutazama upya sera hizo zinazokiuka sharia za kimataifa. 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages