Kundi kubwa la wananchi wa Sudan wamemiminika katika barabara za wilaya moja ya Khartoum kulalamikia kuuliwa raia mmoja na wanajeshi wa nchi hiyo.
Polisi wa kuzuia fujo waliwafungia njia waandamanaji waliokuwa wamebeba bendera za Sudan na nara za mapinduzi katika wilaya ya Burri ya mashariki mwa Khartoum.
Televisheni ya lugha ya Kiingereza ya al Jazeera imeripotihabari hiyo na kuongeza kuwa, maandamano hayo yamefanyika masaa machache baada ya maandamano mengine kuvunjwa na jeshi la polisi mjini Khartoum. Hayo ni maandamano ya kulalamikia kuuliwa raia mmoja katika mji wa el Souk wa jimbo la Sinnar la kusini mashariki mwa Khartoum.
Raia huyo aliuliwa katika machafuko yaliyozuka baada ya wakati wa mji wa el Souk kuandamana kutaka wanamgambo wa serikali waondoke mjini humo. Wakazi wa mji huo na madaktari wamethibitisha tukio hilo na kusema kuwa wanamgambo hao wa serikali wanaoliunga mkono Baraza la Kijeshi la Sudan waliwafhatulia risasi wanaandamanaji na kumuua kwa risasi raia huyo.
Katika ripoti yake, muungano wa madaktari wa Sudan umesema kuwa, watu wanne kati ya wahanga wa mashambulizi hayo ya wanamgambo wa serikali, wanatoka katika familia moja ya Modurman. Taarifa hiyo imeongeza kuwa wanne hao wameuliwa baada ya kupondwa na gari ya wanamgambo hao wa serikali.
Itakumbukuwa kuwa, hivi karibuni wawakilishi wa Baraza la Kijeshi la Mpito nchini Sudan na muungano wa upinzani wa Uhuru na Mabadiliko walitarajiwa kutia saini hati ya makubaliano ya kisiasa saa chache baada ya jeshi hilo kudai kuwa limezima jaribio la mapinduzi.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇