Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kulia) akiwapungia wananchi wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma kufungua Kongamano la Wanawake (UWT) kitaifa, Julai 13, 2019.
Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Gaudencia Kabaka (kushoto) wakati alipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Kigoma kufungua Kongamano la Wananwake Kitaifa, kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma, Julai 13, 2019. Wa pili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga na wapili kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Kigoma, Amandus Dismas Nzamba.
Baadhi ya wananchi wa Kigoma wakimsikiliza Mgeni Rasmi Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza katika Kongamano la Wanawake (UWT) kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika Julai 13, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kulia) akihutubia katika Kongamano la Wanawake (UWT) kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma, Julai 13, 2019.
Majaliwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Gaudencia Kabaka wakitazama hot pot lililotengenezwa kwa mbao wakati alipohutubia katika Kongamano la Wanawake kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma Julai 13, 2019.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇