NA SALVATORY NTANDU.
Watu sita wamefariki dunia na wengine 24 wamejeruhiwa katika ajali iliyotokea usiku wa kuamkia jana katika eneo la nyambula barabara ya kahama kakola kata ya Ngogwa Wilayani Kahama mkoani Shinyanga baada ya Magari mawili kugongana uso kwa uso aina ya Totoya hice yenye namba T 710 AZZ na Toyota Land cruiser yenye namba za usajili T 477 ATC.
Akizungumza na waandishi wa Habari jana mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya kahama,DK George Masasi amekiri kupokea majeruhi hao ambao wanaenelea kupatiwa matibau na miili ya watu sita waliofariki dunia.
Amesema majeruhi watatu wamepewa rufaa ya kwenda kutibiwa katika hospitali ya Bugando kutokana na hali zao kutokuwa nzuri huku majeruhi wengine 19 hali zao zinaendelea vizuri na ambao hali zao zitaimarika wataweza kuruhusiwa kwenda nyumbani.
Nao baadhi ya majeruhi wa ajali hiyo Salu Maige na Martine Marice wamesema dereva wa gari aina ya Hice alikuwa na mwendo kasi ambapo lilimshinda na kusababisha ajali hiyo huku barabara hiyo ikiwa na vumbi kubwa.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya kahama Anamringi Macha ameserikali itaendelea kuchukua hatua kali kwa madereva wanaokiuka sheria za usalama barabarani na kuwataka abiria kupaza sauti ili kudhibiti ajali.
Amesema wamebaini baadhi ya Madereva wa magari ya abiria yaenda vijijini hawazingatii sheria za usalama kwa kuendekeza mwendo kasi huku magari mengine yakiwa ni mabovu hivyo watahakikisha wanasimamia usalama wa abiria kwa kufanya ukaguzi wa mara kwa mara.
Naye kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga (ACP) Richard Abwao amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi na kuahidi kuwa wataanza ukaguzi maalum wa magari yanayoekea katika Halmashauri za Msalala na Ushetu baada ya kubaini uwepo wa taarifa za mwendo kasi kwa madereva.
Amewataja majina waliofariki ni pamoja na dereva wa Hice, Enock maganga(32),Buruan Yasini (32) Mwanamke mmoja na watoto wadogo wa kiume wa wawili na mmoja wa kike wenye umri wa miaka kati ya mitatu hadi mitano ambao majina yao hayajafahamika.
Kamanda Abwao ametoa rai kwa ndugu jamaa na marafiki kujitokeza kuwatambua ili waweze kukabithiwa ndugu zao kwaajili ya tararibu za mazishi.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇