Wawakilishi wanne wa Bunge la Kongresi nchini Marekani wamemuonya Rais Donald Trump wa nchi hiyo kuchukua hatua yoyote ya kijeshi dhidi ya Iran kufuatia kutunguliwa na jeshi la Iran ndege yake ya ujasusi Alkhamisi ya jana, baada ya rais huyo kutoa radiamali kuhusiana na kadhia hiyo.
Katika uwanja huo, Bernie Sanders, ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter akijibu radiamali ya Trump kwamba: "Marekani inatakiwa kufanya mazungumzo na Iran na si kuanzisha vita visivyo na mwisho na vinavyokiuka katiba katika eneo." Naye Ilhan Abdullahi Omar, mjumbe wa bunge la wawakilishi nchini Marekani ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter kwamba: "Kama ilivyokuwa kwa vita vya Iraq, wavamizi wanatumia visingizio visivyo vya kisheria kwa ajili ya kupiga ngoma ya vita sawa na kadhia ya Iraq, watauawa watoto, Wamarekani watapoteza maisha na ulimwengu utakosa usalama."
Aidha Elizabeth Warren, Seneta wa jimbo la Massachusetts akiashiria mzozo kati ya Iran na Marekani ameandika katika mtandao huo wa kijamii kwamba, Trump ndiye mchochezi wa hali hiyo na kwamba siasa zake za kigeni na za ubabe kupitia jumbe zake zenye utata kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter, ndizo zimepelekea kushadidi mgogoro huo. Warren ambaye ni mgombea wa Wademocrat katika uchaguzi ujao wa rais nchini Marekani amebainisha kwamba: "Mimi ninaunga mkono mpango wa kupunguzwa mizozo na tusiwaruhusu watu wanaotaka vita ndani ya serikali hii watuingize vitani." Naye Alexandria Ocasio-Cortez, mwakilishi wa jimbo la New York katika bunge la wawakilishi nchini humo sambamba na kukosoa mienendo hasi ya serikali ya Washington amesema: "Wapenda vita katika serikali ya Marekani wanajaribu kutuvuta katika mapigano ya kijeshi jambo ambalo silo la uwajibikaji kabisa.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇