LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 15, 2019

WAISRAELI WAKUSANYIKA TEL AVIV KUUNGA MKONO UBARADHULI

Makumi ya maelfu ya Waisraeli jana Ijumaa walikusanyika katika mji mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel, Tel Aviv na kufanya matembezi na marasimu ya kuunga mkono ushoga.
Kwa mujibu wa Manispaa ya Tel Aviv, Waisraeli zaidi ya 250,000 walishiriki matambezi na mkusanyiko huo.
Mkusanyiko huo wa kuunga mkono na kushabikia vitendo vya usenge na usagaji unatajwa kuwa mkusanyiko mkubwa zaidi wa kuunga mkono ufuska huo katika eneo la Asia Magharibi (Mashariki ya Kati).
Meya wa Tel Aviv, Ron Huldai amesema mji mkuu huo wa utawala haramu wa Israel unajifakhirisha kwa kuwa mwenyeji wa mkusanyiko mkubwa zaidi wa kuwaunga mkono wasenge, wasagaji na watu waliobadilisha jinsia zao (LGBTQ) katika eneo hili.
Waziri Mkuu wa utawala khabithi wa Israel, Benjamin Netanyahu
Hii ni katika hali ambayo, wiki iliyopita, Waziri Mkuu wa utawala khabithi wa Israel, Benjamin Netanyahu alimteua mwanaharakati ambaye aliwahi kujitangaza hadharani kuwa shoga kwa jina Amir Ohana, kuwa Waziri wa Sheria wa utawala huo haramu.
Utawala wa Kizayuni wa Israel umekuwa ukiwahadaa walimwengu kuwa wao ni kizazi teule cha kihafidhina na kisichojihusisha na vitendo vya ufuska.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages