LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 15, 2019

TANZANIA NCHI YA PILI AFRIKA KUFUNGA MASHINE ZA KISASA ZAKUPIMA MAAMBUKIZI


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (kushoto) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi mtendaji wa EMEA Bw. Helmut Butterweck wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wachangia Damu Duniani yaliyofanyika  kitaifa jijini Mwanza, viwanja vya Furahisha.

Tanzania tunakuwa Nchi ya Pili Afrika kufunga mashine za kisasa za kupima maambukizi ya Damu na makundi ya damu, 
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wachangia Damu Duniani yaliyofanyika  kitaifa jijini Mwanza, viwanja vya Furahisha ambapo Afrika Kusini ndio ya kwanza na sisi tunafuata, Hii ndio Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa chini ya Rais wetu mpendwa John Pombe Magufuli, Serikali ya kuahidi na kutenda, Niendelee kwa kuwaomba watanzania itakuwa haina maana ya kuwa na mashine kama hizi lakini wananchi hawajitokezi kuchangia damu.

Hivyo niombe watanzania kuwa na utamaduni wa kuchangia damu na tuwe na utamaduni wakuchangia damu mara kwa mara ili tuhakikishe wananchi wanao hitaji damu wanapata hasa akinamama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miaka mitano.

 Pia kwa sasa tunaboresha huduma za kibingwa ikiwemo Taasisi ya Upasuaji wa Mifupa  MOI, Upasuaji katika Taasisi ya Moyo ya JKCI na Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Waziri Ummy Mwalimu pamoja na viongozi wa kutoka Wizara ya Afya wakiongea na moja kati ya watu waliojitokeza kuchangia damu, katika Maadhimisho ya Siku ya Wachangia Damu Duniani yaliyofanyika  kitaifa jijini Mwanza, viwanja vya Furahisha.
Baadhi ya picha za Kikundi cha Wasanii wa filamu Tanzania wakionesha igizo kuhusu uhamasishaji kwa jamii juu ya umuhimu wa kuchangia damu, tukio limefanyika kitaifa jijini Mwanza katika viwanja vya Furahisha.
Jopo la watu waliojitokeza kushuhudia Maadhimisho ya Siku ya Wachangia Damu Duniani yaliyofanyika  kitaifa jijini Mwanza katika viwanja vya Furahisha, yaliyofunguliwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.
Mashine kubwa zenye gharama inayokadiriwa kuwa dola za kimarekani 600,000 (laki sita) kila moja ambayo ni sawa fedha za Kitanzania bilioni 1.4, zilizozinduliwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu katika Maadhimisho ya Siku ya Wachangia Damu Duniani yaliyofanyika  kitaifa jijini Mwanza, viwanja vya Furahisha.WAZIRI WA AFYA AHUDHURIA MAADHIMISHO YA SIKU YA WACHANGIA DAMU DUNIANI.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages