NA Lailat Abeid MAELEZO
SERIKALI imesema itaendelea kushirikiana na kampuni za simu ili kuwasaidia wananchi katika mambo mbalimbali ya kijamii yakiwemo ya Afya, Elimu na Miundombinu.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Vodacom Tanzania Foundation, Naibu Waziri wa Tamisemi, Joseph Kandege amesema Serikali itaendelea kuimarisha miundombinu ili kuwawezesha Vodacom kuwafikia watanzania wote wenye mahitaji .
Waziri kandege Amesema Vodacom wanafanya kazi ambazo zinagusa jamii kama afya na kuwasaidia watoto wa kike kwenda shule kwa kuwapatia vitaulo vya kujihifadhia katika hedhi, pia wameendelea kuwasaidia kina mama juu ya ugonjwa wa fistula ambayo inawapelekea wamama wengi kutengwa na jamii.
“ Serikali itahakikisha inaimarisha miundombinu ili kuhakikisha vodacom inawafikia watu wenye uhitaji na pia tumeona jinsi walivyoweza kuwasaidia watoto wa kike na wakinamama wenye fistula juu ya kupata matibabu ya ugonjwa huo na kugawa vitaulo kwa watoto wa kike wenye uhitaji, ambao wanakosa kwenda shuleni pindi wawapo kwenye hedhi”.
Amesema matarajio yake ni kuwa kazi inayofanywa na vodacom iweze kufanywa na mashirika mengine kwa kushiriki jambo kama hilo au kwa kujiunga pamoja na vodacom kufanya jambo hilo.
“ Matarajio yangu kazi hii inayofanywa na Vodacom isiwe yao na hayo mashirika wanayoshirikiana nayo, kwani hili ni jambo la kitaifa, hivyo ni vyema mashirika mengine hata ya watu binafsi wakaendeleza juu ya hili, au wakaanzisha mambo kama haya ilikuweza kusaidia jamii zenye uhitaji kwa ujumla” .
Aidha Mkuurugenzi wa Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation na Afisa Uhusiano, Rosalynn Mwaria amesema wamekuja kuonyesha matokeo chanya ya kazi walizokuwa wakizifanya kuanzia mwaka 2014 hadi 2017, wakiambatana na sekta binafsi pamoja serikali kwa kuwasaidia watoto na kinamama kwenye mambo mbalimbali .
Amesema hadi kufikia hapa wameshawekeza sh bilioni 11 ambazo zimewawezesha kufikia wanawake kwa upande mkubwa na kwa watoto wa kike kwenye sekta ya Elimu , Afya na pia kuwawezesha kiuchumi katika mambo tofauti ili kuiendeleza Tanzania na kuifikia jamii.
Kwa mwaka 2019 hadi 2021, Mkurugenzi huyo amesema wamejikita katika miradi ya watoto katika Elimu na pia kufanya maendeleo ambayo yatawasaidia kutunza mazingira ya Tanzania nzima.
“ Hadi kufikia hapa tumeshawekeza sh bilioni 11 ambazo zimetuwezesha kuwafikia watoto wa kike na wanawake katika kuwasaidia kwenye Afya pamoja na kiuchumi kwa mwaka 2019 hadi 2021, tumejikita katika kuwasaidia watoto wa kike pia kufanya maendeleo ambayo yatatusaidia kutunza Mazingira ya Tanzania.”
Pia amesema watajikita zaidi katika maeneo ya Elimu na kiuchumi kwa ujumla ili kuweza kuwawezesha wafanyabiashara wadogo na wakati ilikuweza kujikwamua kutoka pale walipo ilikuweza kusaidia Taifa kufikia uchumi wa kati kwa mwaka 2025.
“Tutajikita katika maeneo ya Elimu na Uchumi kwa ujumla ili kuweza kuwawezesha wafanyabiashara wadogo na wakati kwa ujumla kujikwamua kutoka pale walipo ilikuweza kusaidia Taifa kufikia Uchumi wa kati mwaka 2025”.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇