Rais wa zamani wa Marekani Jimmy Carter amemshambulia Rais Donald Trump na kusema kuwa uwepo wake katika Ikulu ya White House ni kinyume cha sheria.
Jimmy Carter aliyasema hayo jana Ijumaa na kuongeza kuwa iwapo uchunguzi wa kina utafanyika kuhusiana na madai ya uingiliaji wa Russia katika uchaguzi wa rais wa mwaka 2016, itabainika kuwa Rais Donald Trump hakushinda uchaguzi huo wa rais, lakini hata hivyo akaingia ikulu. Hayo yanajiri katika hali ambayo wakosoaji wengi wa Trump wanasema kuwa alitangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi ambapo Hillary Clinton, mshindani wake wa chama cha Democrat alimshinda kwa karibu kura milioni tatu zaidi.
Katika uwanja huo siku chachhe zilizopita William Barr, Waziri wa Vyombo vya Mahkama nchini Marekani aliwasilisha ripoti ya uchunguzi wa Robert Mueller, mchunguzi maalumu wa faili la madai ya uingiliaji wa Russia katika uchaguzi wa rais wa mwaka 2016 mbele ya bunge la kongresi la nchi hiyo, hata hivyo Wademocrat sambamba na kumtuhumu, walisisitiza kuwa kinyume na madai ya William Barr, ripoti hiyo haimuondolei tuhuma Trump. Inaelezwa kuwa katika ripoti ya Robert Mueller kumetajwa hatua 10 za Trump ambazo zinathibitisha 'ukwamishaji mambo katika mkondo wa utekelezwaji uadilifu.'
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇