Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiongea wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyoitimishwa leo katika viwanja vya Shule ya Msingi Mkapa iliyo katika mji mdogo wa Katoro Mkoani Geita.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Geita Muhandisi Robert Gabriel wakiangalia viatu vya katika banda la Kikundi cha Vijana Cluster cha Shirati Rolya Mkoani Mara wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika leo katika viwanja vya Shule ya Msingi Mkapa iliyo katika mji mdogo wa Katoro Mkoani Geita.
Watoto mbalimbali kutoka Shule zilizoko Mji mdogo wa Katoro Mkoani Geita wakiwa katika maandamano wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika leo katika viwanja vya Shule ya Msingi Mkapa iliyo katika mji mdogo wa Katoro Mkoani Geita.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu Akizindua kitini cha Ajenda ya wajibu wa wazazi wa Malezi na matunzo ya familia Nchini Tanzania wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyoitimishwa leo katika viwanja vya Shule ya Msingi Mkapa iliyo katika mji mdogo wa Katoro Mkoani Geita.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akisoma kitini cha kitini cha Ajenda ya wajibu wa wazazi wa Malezi na matunzo ya familia Nchini Tanzania wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyoitimishwa leo katika viwanja vya Shule ya Msingi Mkapa iliyo katika mji mdogo wa Katoro Mkoani Geita.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu Akizindua Kijarida cha Kisura chenye lengo la kutoa elimu juu ya madhara ya mimba za utotoniwakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyoitimishwa leo katika viwanja vya Shule ya Msingi Mkapa iliyo katika mji mdogo wa Katoro Mkoani Geita.
Na Mwandishi wetu GEITA.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameiagiza mikoa ambayo haijaanzisha mabaraza ya watoto Ncini kufanya hivyo mara moja kama hatua muhimu ya kutekeleza haki ushiriki watoto katika maamuzi mbalimbali yanayohusu haki na ustawi wao.
Waziri Mwalimu amesema hayo leo Mkoani Geita wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyoitimishwa leo katika viwanja vya Shule ya Msingi Mkapa iliyo katika mji mdogo wa Katoro Mkoani Geita.
Ameitaja mikoa ambayo haijaanzisha Mabaraza ya Watoto kuwa ni mikoa ya Tanga, Mbeya, Mtwara, Simiyu Kigoma Mara na Manyara kuitaka kufanya hivyo mara moja ili kutekeleza haki ya ushirikishwaji watoto lakini pia kuimarisha ulinzi wa mtoto hapa Nchini.
Aidha Waziri Ummy ameongeza kuwa katika kuimarisha haki ya ushiriki wa mtoto, Serikali kwa kushirikiana na wadau imeendelea kuhimiza Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuongeza bajeti ya kuwezesha mabaraza ya watoto.
Akitoa ufafanuzi kuhusu Mabaraza hayo Waziri Mwalimu alisema mabaraza hayo yanatoa fursa kwa watoto kujadili masuala mbalimbali yanayohusu haki na ustawi wao na pia kuishauri Serikali kuhusu masuala hayo.
Aidha Waziri Ummy aliongeza kuwa mpaka kufikia mwezi Machi, 2019 serikali ilianzisha mabaraza ya watoto 19 katika ngazi ya mikoa, mabaraza 121 katika ngazi ya Halmashauri za Manispaa,Wilaya,Miji, mabaraza 733 katika ngazi ya Kata na mabaraza 795 katika ngazi ya kijiji,Mtaa akiyataja mabaraza hayo kuwa mchango mkubwa katika kuwajengea watoto uwezo wa kujieleza na kujiamini ambayo ni silaha muhimu katika kujilinda na vitendo vya ukatili.
Waziri Mwalimu ameongeza kuwa kwa hali ilivyo sasa nchini, watoto wengi wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kukatishwa masomo kwa kupewa mimba, kuolewa katika umri mdogo na kutopewa fursa zaidi ya kuendelea kimasomo kwa sababu mbalimbali.
Wzairi Ummy alisisitiza kuwa takwimu za Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Vishiria vya Malaria ya mwaka 2016 inaonyesha kuwepo kwa ongezeko la vitendo vya ukatili dhidi ya watoto hapa nchini hususan wasichana akizitaja takwimu hizi kuonesha kuwa kiwango cha kitaifa kwa ndoa za utotoni ni 37% wakati mimba za utotoni zikiwa 27% na ukeketaji 10%.
Aidha, Takwimu za Jeshi la Polisi za mwaka 2018 zinaonyesha kuwepo kwa matukio 14,419 yaliyoripotiwa katika vituo mbalimbali vya polisi hapa nchini ikilinganishwa na matukio 13,457 kwa mwaka 2017 ambalo ni ongezeko la matukio 1034 sawa na 7.7%.
Waziri Mwalimu ameitaja Mikoa 5 inayoongoza kwa ukatili dhidi ya watoto nchini kuwa ni Tanga (1039), Mbeya (1001), Mwanza (809), Arusha (792) na Tabora (618) huku akiyataja matukio yanayoongoza kwa ukatili kuwa ni Ubakaji (5557), Mimba (2692), Kulawiti (1159), Shambulio (965) na Kujeruhi (705).
Kuhusu ulinzi wa motto Waziri Ummy aliongeza kuwa Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo ya matoto hapa nchini imeratibu uanzishwaji wa Kamati za Ulinzi wa Wanawake na Watoto katika mikoa 26, Halmashauri za Wilaya,Manispaa.Miji na Majiji 176, Kata 1,640 na Vijiji,Mitaa 5,609 akiongeza kuwa kamati hizi zitasaidia kwa kiasi kikubwa kuimarisha ulinzi na usalama kwa wanawake na watoto.
Aidha Waziri Ummy ameongeza kuwa Serikali imeshatoa maelekezo ya kuanzishwa kwa madawati ya ulinzi wa watoto shuleni ili kuboresha mfumo wa upatikanaji wa huduma kwa wahanga wa ukatili na kuimarisha ulinzi wa watoto wawapo shuleni.
Akiongea na Wakati wa Kilele cha Maadhimisho hayo Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel amewaambia wananchi Mkoani mwake kuwa sifa ya mwanaume siyo tu kuzaa watoto bali ni kulinda mke pamoja na watoto kwa kuwapatia mahitaji muhimu na kufanya kazi kwa bidi.
Aidha Mhandisi Gabriel amewataka wanaume kote Nchini kuacha kutafuta heshima baa na badala yake watumie muda mwingi na familia zao ili kuweza kuchangia katika malezi ya watoto ili waweze kufikia ndoto zao.
Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika uadhimishwa kila mwaka ifikapo tarehe 16, Juni na tayari yameitimishwa leo Mkoani Geita katika viwanja vya Shule ya Msingi Mkapa katika Mji wa mdogo wa Katolo na kuitimishwa rasmi na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Ummy Ally Mwalimu.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇