K-VIS BLOG/Masirika ya habari
MOHAMMED Morsi (67), Rais wa Misri aliyepinduliwa mnamo mwaka 2013 na kuwekwa kizuizini amefariki leo Juni 17, 2019 akiwa mahakamani jijini Cairo.
Taarifa za vyombo vya habari vya kimataifa zimesema, Raishuyo wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia kabla ya kuondolewa madarakani na jeshi la nchi hiyo, alianguka akiwa mahakamani na kufariki muda mfupi baadaye.
“Alikuwa anajieleza mbele ya jaji kwa takriban dakika 20, akaanza kuzungumza kwa jazba kabla ya kuanguka. Alikimbizwa hospitalini ambako alifariki baadaye.” Vyanzo vya habari vya mahakama vimedokeza.
Kwa mujibu wa taarifa, Morsi alikuwa na historia ya matatizo ya kiafya ikiwa ni pamoja na kisukari, ini na figo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇