LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 18, 2019

RAIS WA ZAMANI WA UEFA AKAMATWA

Rais wa zamani wa Shirikisho la Soka Ulaya UEFA, Michel Platini amekamatwa kwa tuhuma za rushwa kutokana na nchi ya Qatar kupewa tenda ya kuandaa Kombe la Dunia 2022.

Amekamatwa mapema leo na kuwekwa kizuizini huko Nanterre, Paris, nchini Ufaransa

Amekamatwa ikiwa ni sehemu ya uchunguzi unaoendelea dhidi ya madai ya kuwepo kwa vitendo vya rushwa katika uamuzi wa kukubali michuano ya Soka ya Kombe la Dunia ya mwaka 2022, kufanyika Qatar

Platini, aliyeongoza UEFA tangu mwaka 2007 hadi 2015, kwa sasa atumikia zuio la kutojihusisha na soka kwa miaka minne baada ya kukutwa na hatia ya kupokea rushwa kutoka kwa Rais wa zamani wa FIFA, Sepp Blatter.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages