Rais Dkt. John Magufuli leotarehe 28 Juni, 2019 amefanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wabunge la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) VerĂłnica Nataniel Macamo Dlhovo, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, JobNdugai, NaibuWaziriwa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro na Katibu wa Jukwaa la Wabunge la SADC BoemoSekgoma.
Katika mazungumzo hayo, Dlhovo ambaye ni Spika wa Bunge la Msumbiji amewasilisha salamu za Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi na salamu za Maspika wa SADC pamoja na kueleza kuhusu ushiriki wa jukwaa hilo katika Mkutano wa 39 wa SADC utakaofanyika Jijini Dar es Salaam.
Dlhovo amempongeza Rais Magufuli kwa uongozi mzuri na hatua kubwa ambazo Tanzania inapiga katika maendeleo na ameeleza kuwa Jukwaa la Wabunge la SADC linakusudia kujenga mazingira ambayo yataweka sheria na taratibu zitakazowezesha nchi wanachama kubadilishana uzoefu na kupiga hatua zaidi za maendeleo.
Aidha, Dlhovo amesema Msumbiji na nchi nyingine za Afrika zinatambua mchango mkubwa uliotolewa na Tanzania tangu wakati wa uongozi wa Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere katika ukombozi wa mataifa mengi ya Afrika na uanzishaji wa nchi za mstari wa mbele na SADC.
Kwaupande wake Rais Magufuli amemshukuru Dlhovo kwa kufika Ikulu kumsalimu na kufikisha salamuza Rais Nyusi na Wabungewa SADC na amemhakikishia kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na nchi zote wanachama wa SADC ikiwemo Msumbiji ambayo inauhusiano wa kihistoria na kidugu na Tanzania.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇