Waziri wa Mambo ya Ndani wa Sri Lanka, Vajira Abeywardena amesema kuwa, kwa kuzingatia hali ya usalama iliopo kwa sasa nchini humo, watu hao mbali na kulipa fidia kutokana na kuishi nchini humo kinyume cha sheria, pia wametimuliwa kutoka nchi hiyo. Ameongeza kwamba serikali ya nchi hiyo imeazimia kuangalia upya sheria ya vibali vya kuishi nchini humo sambamba na kuifanya kuwa ngumu zaidi sheria hiyo hususan kwa ajili ya wahubiri wa kidini.
Hata kama Waziri wa Mambo ya Ndani wa Sri Lanka hakutaja utaifa wa raia waliotimuliwa, lakini viongozi wa polisi wamesema kuwa akthari ya raia hao wa kigeni wanatoka nchi za India, Pakistan, Bangladesh na Maldives. Tangu mwezi uliopita Sri Lanka imetangaza hali ya hatari ambapo imetoa idhini kwa maafisa usalama kumtia mbaroni mshukiwa yeyote. Mji wa Colombo ulikumbwa na mashambulizi ya kigaidi tarehe 21 Aprili mwaka huu ambayo yaliyalenga makanisa na hoteli za mji huo na kusababisha watu 253 kuuawa na wengine zaidi ya 500 kujeruhiwa. Baadaye kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS) lilidai kuhusika na jinai hiyo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇