LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 5, 2019

DK. BASHIRU AWAFUNDA UVCCM KUHUSU KUJIZATITI KATIKA MAPAMBANO YA KUIKOMBOA TANZANIA KIUCHUMI

Dodoma, Tanzania
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Bashiru Ally (Pichani), amesema  CCM, imejikita katika masuala ya Kilimo na Viwanda, Ulinzi na Usalama, Sayansi na Teknolojia katika muktadha wa mapambano ya kujikomboa kiuchumi na mwelekeo wa siasa za kidunia.

Akizungumza katika Mkutano Maalum wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Katibu Mkuu amesema katika mazingira ya sasa ya kidunia CCM inatambua kuwa mapambano ya kiuchumi yamejikita katika namna ambayo nchi masikini lazima zihakikishe zinasimamia ipasavyo sekta ya kilimo, uzalishaji wa wenye tija sanjari na viwanda vitakavyochakata bidhaa za kilimo na kujenga uwezo wa kuzalisha chakula cha kujitosheleza na ziada.

Kuhusu unyeti wa suala la ulinzi na usalama Dk. Bashiru amesema, wananchi na hasa vijana ndiyo walinzi wa mstari was mbele, hivyo uzalendo, nidhamu, kufanya kazi, utii na kujituma ni misingi muhimu kwa vijana wa CCM. 

Aidha, ameeleza kuwa jitihada  za Tanzania kujikomboa kiuchumi hazitapokelewa vizuri na maadui ambao wako ndani na nje ya nchi, hivyo vijana wa Kitanzania wana jukumu la kuilinda, kutetea msimamo na kuyasemea mazuri yanayofanywa na Serikali.

Kuhusu Sayansi na Teknolojia Dk. Bashiru Katibu ameeleza wigo wa uwanda huo kuwa ndio ulipo uwanja wa mapambano na ni muhimu kujihami mapema na kuwa tayari kukabiliana mashambulizi ya wanaotumia mitandao kupotosha kazi nzuri inayofanyika katika Tanzania, kwa kuwajibu kwa hoja na kwa ushahidi wakati wote.

Dk. Bashiru amewataka wajumbe wa Mkutano Maalum wa Baraza Kuu la UVCCM kutoa aina ya Kiongozi (Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa kutoka vijana) ambaye anaelewa mazingira yaliyopo na awe tayari kusimama imara kuulinda Muungano, kujenga umoja, kulinda uhuru.

Awe mtu mwenye msimamo usioyumba, atakayelinda heshima ya viongozi  na anayeakisi maono na mwelekeo wa Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. John Magufuli.

Amesema, vilevile lazima awe mpanbaji dhidi ya vitendo vya ukabila, udini, ubaguzi wa rangi, rushwa, kila jambo linalokwenda kinyume na Katiba, Kanuni na desturi nzuri za CCM ili visiwe na nafasi katika Umoja wa Vijana wa CCM

Mkutano Maalum wa Baraza Kuu la UVCCM ulifanyika jana mjini Dodoma, kuchagua Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC), anayewakilisha UVCCM, baada ya nafasi hiyo kuwa wazi.

Mbali na Katibu Mkuu wa CCM mkutano huo wa aina yake umehudhuriwa  pia na  Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Humphrey Pokeoole, Mzee Kombo (Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM) na na Mwenyekiti wa UVCCM, Kheri James.


2 comments:

  1. An impressive share! I have just forwarded this onto a
    colleague who has been conducting a little research
    on this. And he actually bought me breakfast due to the fact that
    I found it for him... lol. So let me reword this....
    Thank YOU for the meal!! But yeah, thanks for spending some time to talk
    about this topic here on your website.

    ReplyDelete
  2. hi!,I like your writing very a lot! proportion we keep up a correspondence extra approximately your article on AOL?
    I require a specialist on this space to unravel my problem.

    Maybe that's you! Taking a look forward to look you.

    ReplyDelete

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages