Rais Dk. John Magufuli akipokea mfano wa hundi ya Sh. Bilioni 2.1 za Gawio la Serikali, kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL Waziri Kindamba, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL Omar Nundu katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Shirika hilo jijini Dar es Salaam, leo. Picha na Ikulu.
Na Paschal Doto, Dar es Salaam
Rais Dk. John Magufuli ametoa siku 30 kwa Ikulu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara zote, Viongozi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma, kutumia huduma zote za Kampuni ya Mawasiliano ya Simu Tanzania (TTCL) ili kupanua huduma za mawasiliano ya Mtandao wa Kampuni hiyo nchini.
Akizungumza wakati wa Hafla ya kukabidhi gawio kwa Serikali la Sh. Bilioni 2.1 kutoka TTCL, Rais Magufuli alimtaka Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo kumuorodheshea namba za simu za Viongozi na Watendaji wote wa Serikali ikiwemo Mawaziri na Makatibu Wakuu kuona kama wanatumia laini za simu za TTCL.
Aliongeza kuwa tangu atoe agizo lake mwaka jana, kuhusu matumizi ya huduma za mawasiliano ya TTCL katika Ofisi mbalimbali za Umma, hakuna Ofisi yoyote ilitekeleza agizo hilo ukiondoa baadhi ya Taasisi chache ikiwemo Jeshi la Wananchi Tanzania na Jeshi la Polisi.
"Nimefurahi alipokuwa akitaja Taasisi na Mashirika ambayo yamejiunga moja kwa moja na kutumia huduma za TTCL, nilisikitika sana niliposikia Ofisi yangu haikutajwa, pia Ofisi ya chama changu cha CCM, sasa kama wamesikia na wako hapa nataka kipindi cha mwezi mmoja tuanze kutumia simu za TTCL", alisema Rais Magufuli.
Rais Magufuli alizitaka Ofisi zingine za Serikali kutumia huduma za Kampuni hiyo ya Mawasiliano Nchini ili kuinua na kuimarisha utendaji kazi wake katika nyanja mbalimbali za maendeleo nchini na kuzitaka Taasisi zingine ziige mfano huo kwa vitendo na siyo maneno.
" Si Ofisi ya Makamu wa Rais, Si Ofisi ya Waziri Mkuu, Si Ofisi ya Rais, Si Wizara ya Fedha, hata Wizara yako ya Mawasiliano na Uchukuzi nayo haijatajwa hapa, nataka kusema tusipounga mkono, vyetu tutachezewa mno, tusipowaimarisha hawa TTCL, hawatafika mbali, lakini wakipata ushirikiano matokeo tutayaona", alisema Rais Magufuli.
Rais Magufuli alieleza kuwa kabla ya Shirika hilo halijarudishwa Serikalini, katika kipindi cha miaka 15 kutoka mwaka 2001 TTCL ilikuwa ikipata hasara ya Sh Bilioni 15 kila mwaka, huku likishindwa kutoa gawio lolote kwa Serikali.
"Wakati Shirika hili likiendeshwa na Wabia wetu, lilikuwa halitoi gawio lolote, lakini pia lilikuwa likipata hasara ya Bilioni 15 kwa mwaka, kwa hiyo mnaweza mkaelewa hii ina maana gani kwenye uchumi wa nchi, hivyo basi kuweza kufikia hatua hii ya kupata faida ya Sh.bilioni 8.3, na kuweza kutoa gawio la Serikali Sh. Bilioni 2.2 ni mafanikio makubwa", alisema Rais Dkt Magufuli.
Pia Rais Magufuli alisema kuwa Sekta ya Mawasiliano kwa sasa imepanuka nchini na kuwezesha sekta nyingine kufanya kazi kwa ufanisi kwani katika sekta mbalimbali kwa sasa sekta hii inahitajika sana.
" Sekta ya Mawasiliano imesaidia kukua kwa sekta nyingine kama sekta ya fedha, ambapo mwaka jana miamala ya fedha ilifanyika kwa njia ya kimtandao ilikuwa na thamani ya Sh Trilioni 139.2 sawa na Trilioni 11.6 kwa mwezi.
Lakini pia sekta ya mawasiliani ni kichocheo kikubwa kwa Sekta za Elimu, Afya, Biashara, Kilimo, Viwanda Ufugaji, Utalii na Ujenzi", Alisema Rais Magufuli.
Your Ad Spot
May 21, 2019
Home
featured
Uchumi
RAIS MAGUFULI ATOA SIKU 30 KWA VIONGOZI NA WATENDAJI WAKUU WA SERIKALI KUTUMIA HUDUMA ZA KAMPUNI YA TTCL.
RAIS MAGUFULI ATOA SIKU 30 KWA VIONGOZI NA WATENDAJI WAKUU WA SERIKALI KUTUMIA HUDUMA ZA KAMPUNI YA TTCL.
Tags
featured#
Uchumi#
Share This
About Bashir Nkoromo
Uchumi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇