LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 9, 2019

MARUFUKU KUINGILIA TAALUMA ZA MADAKTARI

Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amepiga marufuku wanasiasa kuingilia fani za taaluma za madaktari, wakunga na wauguzi nchini.

Ummy ameyasema hayo bungeni wakati akihitimisha hotuba ya bajeti ya wizara yake, ambapo amesema kama daktari, muuguzi au mkunga amekosea wapelekwe kwenye mabaraza yao ambayo ndiyo yanashughulikia suala la nidhamu kwa kada hiyo ya wstumishi.

“Kutokana na hali halisi ilivyo, muuguzi mmoja anafanya kazi ambayo ingefanywa na wauguzi watano na madaktari wanafanya kazi hivyo si vema kuwakatisha tamaa.

“Sisi kwa kutambua umuhimu wao tutaendelea kuwatetea wauguzi na madaktari wetu, tusiwakatishe tamaa na isitoshe hao wenye fedha hawaendi kutibiwa kwenye hizo hospitali za Serikali, matokeo yake wanaoumia ni watanzania,” amesema Waziri Ummy.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages