Waziri Mkuu wa Iraq amewasili hapa nchini mapema leo katika ziara yenye lengo la kuimarisha uhusiano wa pande mbili wa Tehran na Baghdad.
Baada ya kuwasili mjini Tehran, Adil Abdul-Mahdi amepokewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Mohammad Javad Zarif katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Mehrabad.
Waziri Mkuu wa Iraq tayari amepokewa na mwenyeji wake Rais Hassan Rouhani, na wawili hao wanatazamiwa kushiriki mazungumzo juu ya kuimarisha uhusiano wa pande mbili katika nyuga mbalimbali.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Iran Press, ujumbe wa ngazi za juu wa Iraq uliwasili hapa nchini Jumanne iliyopita, kwa ajili ya maandalizi ya safari hii ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo.
Machi 27, Rais Hassan Rouhani alifanya mazungumzo ya simu na Adil Abdul-Mahdi, Waziri Mkuu wa Iraq, ambapo aliemuleza matumaini yake ya kutekelezwa haraka makubaliano yaliyosainiwa kati ya Iran na Iraq, wakati wa safari ya Dakta Rouhani mjini Baghdad hivi karibuni.
Hii leo, mabadilishano ya kibiashara kati ya Tehran na Baghdad yana thamani ya takriban dola bilioni 12 za Marekani.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇