watu 50 wameuawa katika shambulio la wavamizi waliobeba silaha kaskazini magharibi mwa Nigeria.
Habari hiyo iliripotiwa jana Ijumaa na Spika wa Bunge la Jimbo la Zamfara, Sunusi Rikiji ambaye aliongeza kuwa, mauaji hayo yalifanyika Jumanne iliyopita katika kijiji cha Sakajiki, eneo la Kauran Namoda jimboni Zamfara.
Amesema wanakijiji walikusanyika na kukabiliana na wezi wa mifugo, ambapo watu 50 waliuawa katika makabiliano hayo huku wengine kadhaa wakijeruhiwa.
Mwezi uliopita, wavamizi waliokuwa juu ya pikipiki waliwaua kwa kuwapiga risasi watu 32 katika kijiji cha Kware, wilayani Shinkafi katika jimbo hilo hilo la Zamfara.
Asasi mbalimbali zimezitaka pande zote zinazopigana katika jimbo hilo nchini Nigeria kuwalinda raia na kuheshimu sheria za kimataifa.
Takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonyesha kuwa, zaidi ya watu milioni saba wanahitajia misaada ya kibinadamu kaskazini mashariki mwa Nigeria.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇